Miaka 20 ya azimio namba 1325: Mafanikio na Changamoto
Mwaka huu azimio namba 1325 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake na ulinzi na usalama duniani, limetimiza miaka 20 tangu kupitishwa kwake.
Mwaka huu azimio namba 1325 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake na ulinzi na usalama duniani, limetimiza miaka 20 tangu kupitishwa kwake.
Filamu mpya iliyopewa jina, “Zuia ndoa za utotoni Sudan Kusini” imeoneshwa kwa mara ya kwanza kwa wanajamii katika eneo la Yambio jimboni Equatoria Magharibi ikiwa na lengo la kupambana na unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro pamoja na ubakaji ambavyo ni matukio ya kawaida katika nchi hiyo changa zaidi ulimwenguni.
Ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa malengo ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake miaka 75 ya uwepo wake, kuwa mtetezi mkubwa wa amani na haki za wanadamu kote duniani, nchini Sudan Kusini, mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS umeshirikiana na Jeshi la wananchi wa Sudan Kusini SSPDF kuwapa mafunzo wakufunzi kuhusu kuzuia ukatili wa kingono unaohusiana na mizozo.
Kamati ya tuzo ya amani ya Nobel yenye makao yake nchini Norway leo imelitangaza shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kuwa ndio mshini wa tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huuu wa 2020.
Ripoti yenye kurasa 46 iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNCHRSS, imeeleza kuwa Sudan Kusini tangu ilipopata uhuru wake mwaka 2013, mzozo wa kikatili nchini humo umesababisha mateso yasiyoweza yasiyopimika kwa raia na kusababisha kiwango viwango vya kutisha vya ukosefu wa chakula na utapiamlo hali ambayo inatumiwa kama mbinu ya vita.
Wanawake wakimbizi wa ndani kwenye eneo la Malakal nchini Sudan Kusini wanasema wamechoshwa na vita na kupoteza watoto wao kila uchao, sasa wanaitaka serikali kupanda mbegu ya amani na kusikiliza vilio vyao japo mara moja.