Tunakufa kwa njaa. Tunahitaji chakula-Sudan Kusini
Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP linasema hali ya kibinadamu nchini Sudan Kusini inaendelea kuzorota kwa kasi wakati wimbi la njaa likienea katika nchi ambayo ina mgogoro, mvua kubwa na mafuriko ambayo yanavuruga upatikanaji wa chakula kwa watu.