Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

DR Congo

Karatasi ya plastiki imetenganisha mama na mwanae atika kituo cha matibabu ya ebola Beni, Kivu Kasakzini nchini DRC.
© UNICEF/Thomas Nybo

Ebola DRC: UNICEF yachukua hatua kudhibiti kuenea 

Kufuatia serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kutangaza kifo cha mtu mmoja huko Butembo jimboni Kivu Kaskazini kutokana na ugonjwa wa Ebola, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limepeleka wafanyakazi zaidi na linajiandaa kupeleka vifaa vya matibabu. 

Viongozi wa kituo cha yatima cha Mungu ni Mwema huko Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto na walinda amani kutoka Tanzania baada ya kupokea msaada.
TANZBATT_7/ Issa Mayambua

Nikiondoka watoto yatima DRC wataishi namna gani? - 'Mama Noela'

Noela Kombe al maaruf Mamaa Noela  ni mwanamke shujaa aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa kujitolea kulea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu licha  ya kuwa na changamoto nyingi anazo kumbana nazo wakati wa uendeshaji wa kituo  hicho cha Mungu ni Mwema kilichopo eneo la Beni mjini jimboni Kivu kaskazini nchini jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.