Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

DR Congo

Francine na watoto wake watatu walilazimika kuondoka kijijini kwake kutokana na mzozo usiokoma mashariki mwa DRC. Sasa wanapokea msaada wa WFP katika kambi ya wakimbizi wa ndani huko Kivu Kaskazini.
© WFP/Michael Castofas

WFP DRC waomba msaada wa $Mil 425 kusaidia wakimbizi wa ndani

Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao. 

Sauti
1'49"