Nikiondoka watoto yatima DRC wataishi namna gani? - 'Mama Noela'

1 Februari 2021

Noela Kombe al maaruf Mamaa Noela  ni mwanamke shujaa aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa kujitolea kulea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu licha  ya kuwa na changamoto nyingi anazo kumbana nazo wakati wa uendeshaji wa kituo  hicho cha Mungu ni Mwema kilichopo eneo la Beni mjini jimboni Kivu kaskazini nchini jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC. 

Kituo hicho cha Mungu ni mwema kinacho hudumia watoto zaidi ya 30, B Noela Kombe anaeleza kuwa uamuzi wa kulea watoto hao ulianza tangu akiwa binti wa miaka 15 ambapo mpaka sasa amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miongo 3 na hii ni kutokana  na nia yake ya kutaka kusaidia watoto wasio jiweza wakiwemo yatima.  

Kufuatia uamuzi wake wa kujitolea  kulea watoto hao amesema  juhudi hizo zimezaa matunda kwani mpaka sasa baadhi yao wanasoma shule za msingi na Sekondari na wengine wanajitegemea na Maisha yao. 

Ameeleza changamoto mbalimbali zinazo mkabili  kuwa ni pamoja na ukosefu wa makazi bora ya kuishi kwa watoto hao mavazi na chakula. 

Pamoja na changamoto hizo amepongeza  walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika kikosi cha kujibu mashambulizi cha FIB MONUSCO jimboni kivu kaskazini nchini DRC kwa kutoa misaada ya kiutu na kinadamu. 

Kwa upande wa watoto  wanaolelewa katika kituo hicho wamemshukuru mama huyo kwa kazi kubwa ya kuwalea na kufikia hatua ya kujitambua. 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter