Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

DR Congo

Viongozi wa wanawake DRC wakiwakilisha  sekta zote za asasi za kiraia, wakiwa na Leila Zerrougui, Mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO
MONUSCO/John Bompengo

Inasikitisha baadhi ya raia wa DRC hawatashiriki uchaguzi huu muhimu-Bi Zerrougui

Leila Zerrougui, Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, amesema kuwa anasikitika kwamba kuna raia ambao hawataweza kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaofanyika jumapili hii ya tarehe 30 mwezi huu wa Desemba nchini humo, kufuatia uamuzi wa Tume Huru ya Taifaya uchaguzi ya nchi hiyo, CENI, kuahirisha upigwaji kura katika maeneo ya Beni, Butembo na Yumbi kwa sababu ya mlipuko wa Ebola na ukosefu wa usalama.

 

Kutoka kushoto: Bendera ya UN ikipepea New York; Naibu Katibu Mkuu akiwa na nakala ya ripoti ya  UNCTAD; Walinda amani wa UN; Katibu Mkuu akiwa na wanawake viongozi waandamizi wa UN
UN

Zilizovuma mwaka 2018

Mwaka 2018 ulighubikwa na changamoto nyingi hususan kwa nchi za Afrika, mizozo ikiendelea kukumba bara hilo sambamba na magonjwa. Hata hivyo kulikuwa na habari chanya, na kwa muhtasari tutaangazia pande zote za sarafu wakati huu ambapo tunafunga mwaka huu wa 2018.

 

Shirika la chakula duniani, WFP likisambaza mgao wa chakula katika jimbo la Ituri, DRC ambako maelfu ya watu wamekimbia machafuko ya kikabila mnamo 21 Machi 2018.
WFP/Jacques David

Idadi ya waliofikishiwa msaada na WFP nchini DRC mwaka 2018 imeongezeka maradufu

Kadri machafuko yalivyozidi kuenea mwaka 2018, pamoja na idadi kubwa ya watu waliopoteza makazi na kiwango kidogo cha  mavuno kilichoambatana na umaskini, hali iliyosababisha idadi ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,  DRC kufikia milioni 13.1, shirika la mpango wa chakula duniani WFP lililazimika kuongeza operesheni zake nchini  humo na kufikia watu milioni 5.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya  ICC
UN Photo/Rick Bajornas)

DRC Jiepusheni na uhalifu wakati wa uchaguzi la sivyo mtawajibishwa- ICC

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC tarehe 23 mwezi huu, mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC imeonya kuwa yeyote yule nchini humo ambaye atachochea, ama atashiriki katika fujo kwa kuamuru, kutaka ama kuhimiza au kuchangia kwa njia yoyote ile au kutenda makosa yaliyo chini ya mamlaka ya ICC atashtakiwa na kufikishwa mbele ya mahakama.