Walinda amani wa TANZBATT-7 watoa zawadi kwa watoto yatima DRC.
Walinda amani wa TANZBATT-7 watoa zawadi kwa watoto yatima DRC.
Amani na Usalama
Walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu katika kikundi cha TANZBATT-7 ambacho kiko katika kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB, cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO, wametembelea na kutoa zawadi kwa watoto wa kituo cha Mungu ni mwema, Beni, DRC.
Msaada huo wa vyakula na mahitaji mengine ya kibinadamu umepokelewa kwa furaha na watoto ambao wanalelewa katika kituo cha Mungu ni mwema. Mwanahabari Luteni Issa Mwakalambo, Afisa habari wa TANZBATT-7 ameshuhudia tukio hilo na anaeleza zaidi.