Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

DR Congo

Wanawake wakiwa wamekusanyika katika kituo cha kugawa chakula cha Nyanzale Kivu Kaskazini DRC. Kituo hicho kinawalenga kwa msaada familia zisizojiweza na zilizo hatarini
OCHA/Ivo Brandau

Mashirika ya UN yaendelea kufikisha nuru kwa wakimbizi huko Ituri DRC 

Katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake umeendelea kusambaza misaada kwa wakimbizi wa ndani ambao walilazimika kukimbia makwao na kuacha kila kitu na hivi sasa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi hususan katika eneo la Pinga jimboni humo. Misaada hiyo imekuwa jawabu kwa wakimbizi ugenini.

Sauti
2'35"
Anwarita akiwa nyumbani kwa wazazi wake walezi huko Bona, jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
© UNICEF/Roger LeMoyne

"Nilisikia sauti usiniache! ndipo nikakuta mtoto Anuarita"- Asema baba aliyenusuru mtoto msituni huko DRC

Anwarita mtoto mwenye  umri wa miaka 8 amejikuta yatima baada ya waasi kuua kwa mapanga wazazi wake huko Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Hivi sasa Anwarita anaishi na familia iliyomnusuru msituni, wakati huu ambapo takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema kwa sasa watoto milioni 3 nchini humo wametawanyishwa na mizozo.
 

Wasichana wakibeba maji Yangambi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC.
CIFOR/Axel Fassio

Pamoja na magumu wanayopitia, raia wa DRC waonesha mshikamano

Ikiwa leo ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA inapatia nchi wanachama wa Umoja huo hali halisi ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, , raia nchini humo licha ya machungu wanayopitia na madhila yanayowakabili  wameendelea kuonesha mshikamano wa ajabu baina yao ili angalau kupunguza machungu wakati jamii ya kimataifa ikihana kuwanusuru.

Sauti
2'32"