Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Makala Maalum

Picha ya maktaba ikionesha WHO na wadau wengine walipopeleka msaada wa kudhibiti ugonjwa wa surua katika eneo la West Darful mwezi April 2015 nchini Sudan. Huduma kama hiyo sasa iko katika majimbo ya Sudan Kusini
WHO Sudan

Umuhimu wa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa katika wakati huu wa janga la Corona

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa  limechukua jukumu muhimu katika kukabiliana na janga la COVID-19, tangu mgonjwa wa kwanza alipotangazwa katika mji wa China,  Wuhan mnamo mwezi Desemba mwaka jana 2019. Kwenye mkutano na waandishi wa habari  mkuu wa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, anazitaja sababu tano za umuhimu wa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa  katika wakati huu wa Janga la Corona kuwa ni: 

Picha ya juu ikionesha mtaa wa mabanda wa Mathare mjini Nairobi Kenya
UN-Habitat/Julius Mwelu

Maji ni muhimu ili makazi duni Kenya yadhibiti COVID-19

Lengo namba 6 la malengo ya maendeleo endelevu, SDG, linalenga kufanikisha upatikanaji wa maji kwa wote na kwa usawa ifikapo mwaka 2030. Lakini bado ulimwenguni kote, kama ripoti ya maendeleo ya maji ya Umoja wa Mataifa, ilivyoonesha, mabilioni ya watu bado wanakosa maji safi na salama na huduma za kujisafi na watu wanaachwa nyuma kwa sababu mbalimbali ikiwemo  ubaguzi kwa misingi ya jinsia, kabila, tamaduni na hali ya kijamii.

 

Mpishi Ron Pickarski akikatakata mboga jikoni kwake Boulder Colorado
©FAO/Benjamin Rasmussen

COVID-19 ikitikisa, mlo uwe vipi?

Wakati wazazi wengi wanatafuta milo iliyokwishapikwa tayari na vyakula vya kusindikwa kama njia ya haraka na ya bei nafuu ya kulisha familia, kuna njia mbadala rahisi, za bei nafuu na zenye afya  hasa wakati huu wa ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19

Watoto wa shule sehemu za Beni -DRC wajifunza kuwa kuosha mikono ndiyo njia bora ya kujilinda dhidi ya magonjwa ikiwemo Ebola
UNICEF/Thomas Nybo

Jinsi ya kuzungumza na watoto kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona

Ni rahisi sana kuhisi kuzidiwa uwezo na kila kitu pindi unaposikia kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19. Ni wazi kuwa watoto wanapata shaka na shuku hasa wanapoona taarifa kwenye runinga au kusikia kutoka kwa watu. Je utazungumza nao vipi? Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limekupatia vidokezo vifuatavyo ili uweze kuibua mjadala na watoto na kuzungumza nao.

Mtoto wa umri wa miezi mbili apokea cheti cha kuzaliwa mjini Accra,Ghana.
UNICEF/Frank Dejongh

Usajili wa kuzaliwa ni nini na una umuhimu gani?

Katika nchi nyingine, usajili wa kuzaliwa haupewi kipaumbele kama jambo la kawaida kufuatia kuzaliwa kwa mtoto. Lakini kwa wengine wengi, ni hatua muhimu inayokosekana katika kuthibitisha utambulisho wa kisheria wa mtoto. Bila huo, watoto hawatambuliki na serikali zao, hivyo haki zao zinaweza kutolindwa na kutozingatiwa, pamoja na huduma muhimu kama huduma za afya na elimu.

Karibu robo ya watoto wote waliozaliwa duniani walio chini ya wa miaka 5 hawajawahi kusajiliwa. Maisha ya watoto hawa ni muhimu, lakini hawawezi kulindwa ikiwa serikali hawatambui.

Katika viunga vya mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott, bustani ya mapangaboi ya kuzalisha umeme kwa njia ya upepo  yanaonekana kwa mbali na ni jawabu sahihi katika kuwa na nishati rejelezi
UNDP Mauritania/Freya Morales

Safari ya kuanzia UNFCCC hadi COP25:

Mabadiliko ya tabianchi yanatokea. Joto duniani sasa hivi ni nyuzi joto 1.1 zaidi ya ilivyokuwa mwanzoni mwa mapinduzi ya viwanda, na tayari linaleta madhara makubwa kwa ulimwengu, na kwa maisha ya watu. Ikiwa kiwango cha sasa kitazidi, basi kiwango cha joto duniani kinaweza kuongezeka kwa nyuzi joto 3.4 hadi 3.9 kwenye kipimo cha selsiyasi katika karne hii, kiwango ambacho kinaweza kusababisha madhara makubwa zaidi na yenye uharibifu kwa tabianchi.