27 Machi 2020

Askari wengi wameona vitisho vya vita kwa haraka, na ingawa ilikuwa ya kutisha mara nyingi, walijua ni nani wanapigana naye, na wangeweza kumtambua adui wao. 

Andiko la Waziri wa afya wa Kenya Mutahi Kagwe na Siddharth Chatterjee, Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya. 

COVID 19 au Virusi vipya vya Corona ni tofauti. Katika virusi hivi, adui haonekani na wakati mwingine anasababisha kifo, na kazi ya kukabiliana na janga hili ni ngumu zaidi.

Karibu karne moja iliyopita gonjwa la homa ya Uhispania liliwaua watu takriban milioni 50, zaidi ya majeruhi wote wa pamoja wa Vita vya dunia vya kwanza na vya pili. Uelewa wetu juu ya maambukizi ya magonjwa na matibabu uko mbele sana kwa msimamo wetu  wa mnamo mwaka 1918, lakini virusi mpya  vya corona  vimeonyesha kikomo cha uwezo wetu wa kukabiliana na mlipuko wa magonjwa.

Ushauri wa kujikinga ni wazi: osha mikono yako vizuri na mara nyingi, jitenge mwenyewe ikiwa unahisi kuwa una dalili, dumisha umbali wa kijamii, epuka kadamnasi na pia maeneo ya umma ikiwa dalili zako zinaongezeka, wasiliana na huduma za matibabu. Ni kwa kufuata ushauri huu ambapo tunaweza kutegemea kumaliza wimbi la maambukizi mapya.

Kwa sasa,  virusi vinaenea na kwenye mstari wa mbele kati ya umma ulio na uoga na wale walio na jukumu la kuelekeza la kufanya, wafanyakazi wa huduma ya afya ambao sisi sote tunategemea wanaweza kusahaulika kwa urahisi.

Wakati wa milipuko ya Ebola miaka sita iliyopita, Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO, lilikadiria kuwa wafanyikazi wa afya walikuwa kati ya mara 21 na 32 ya uwezekano wa kuambukizwa Ebola kuliko watu wengine katika idadi ya watu wazima. Huko Afrika Magharibi wafanyakazi wa huduma za afya zaidi ya 350 walikufa wakipiga vita Ebola.

Madaktari, wauguzi, walezi na huduma za matibabu ulimwenguni kote wanakabiliwa na mzigo mkubwa mno katika vituo vya afya.Wanafanyakazi katika mazingira yanayofadhaisha na ya kutisha, sio kwa sababu virusi havieleweki, lakini kwa sababu wanafanya kazi katika mazingira ambayo hayana vifaa au dawa, wanafanya kazi sana na wao wenyewe wana hatari ya kuambukizwa.

Hatari kwa madaktari, wauguzi na wengine kwenye mstari wa mbele imekuwa wazi:  Nchini Italia takribani madaktari 18 wenye ugonjwa wa corona wamefariki dunia. Uhispania iliripoti kwamba zaidi ya wafanyakazi wa huduma za afya zaidi ya 3,900 wameambukizwa. 

Tunahitaji azimio lote la jamii ambayo hatutawaruhusu askari wetu wa mstari wa mbele kuwa wagonjwa. Lazima tufanye kila kitu kusaidia wafanyikazi wa afya ambao, licha ya uoga wao wenye msingi, wanaingia moja kwa moja kwenye njia ya COVID-19 kuwahudumia walioteseka na kusaidia kuzuia kuenea kwa virusi.

Katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, kama ilivyo katika maeneo mengine, shinikizo kwa nguvu ya wafanyakazi wa afya litaongezeka katika miezi ijayo. Utafiti wa hivi karibuni wa wanachama wa National Nurses United (NNU) nchini Marekani, umebaini kuwa ni asilimia 30 pekee waliamini shirika la huduma ya afya lilikuwa na idadi ya kutosha ya vifaa vya kinga ya kibinafsi (PPE) la kukabiliana na tukio la upasuaji. Katika sehemu zingine za Ufaransa na Italia, hospitali hazina barakoa na hivyo basi kulazimisha madaktari kuchunguza na kutibu wagonjwa wa corona bila kinga ya kutosha.

Hali katika nchi masikini itakuwa mbaya zaidi. Mahitaji ni mengi kupindukia. Nchini Kenya ili kuwezesha wafanyikazi wa afya kufanya kazi zao salama tutatoa vitu muhimu kama vile gauni, glavu, barakoa matibabu, na pia tutapeana  ujuzi na habari zaa corona zinapozuka. Kama washirika Serikali ya Kenya, Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa wameazimia kuchunguza kila njia kuhakikisha msaada wote unaowezekana kwa wafanyikazi wa afya.

Ushahidi unaonyesha kuwa virusi vya corona vinaweza kuishi kwenye sehemu yoyote  kwa hadi siku tatu, lakini pia huuliwa kwa urahisi na dawa maalum. Wafanyikazi wa afya wanahitaji msaada wa wafanyakazi wa kusafisha sehemu zote hospitalini. Hatua kama hizi zinaweza kutoa uhakikisho unaohitajika kwa watoa huduma waliosisitiza na kulinda umma pia.

Kama askari, wafanyikazi wa afya pia wanakabiliwa na mafadhaiko makubwa ya kiakili. Mara nyingi inasahaulika kuwa kama wanadamu, wanahisi huzuni ya kupoteza wagonjwa wao.Wao pia wana familia, na kwa kawaida pia wataogopa kwamba virusi vinaweza kuwafikia wale wanaowapenda zaidi.

Wakati wowote inapowezekana tutahakikisha wafanyikazi wa huduma ya afya wanapata huduma za ushauri nasaha wanaweza kugharimia kabla ya kuendelea tena, kwa kuwa hii inaweza kuwa vita ya muda mrefu.
Tunahitaji pia kutumia habari sahihi kama njia ya kujitetea. Mapotofu yanaweza kusababisha hofu ya umma, tuhuma na machafuko; inaweza kuvuruga upatikanaji wa chakula na vifaa muhimu na kugeuza rasilimali - kama vile barakoa - mbali na wafanyikazi wa afya na wafanyikazi wengine wa mstari wa mbele ambao wanahitaji kubwa zaidi.

Covid-19 haitakuwa hatari ya mwisho tunayoshuhudia. Ushujaa, kujitolea na kutokuwa na ubinafsi kwa wafanyakazi wa matibabu huruhusu sisi wengine kiwango cha uhakikisho kwamba tutashinda virusi hivi.

Lazima tuwape wafanyakazi hawa wa afya msaada wote wanaohitaji kufanya kazi zao, kuwa salama na kuwa hai. Tutazihitaji wakati janga linalofuata litakapotokea.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter