Simulizi Yangu: Kukabili usafirishaji haramu Malawi
Maxwell Matewere, mtaalamu katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuzuia uhalifu na madawa ya kulevya, (UNODC) nchini Malawi, amekuwa akiendelea na harakati zake za kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu kwa zaidi ya miongo miwili. Leo hii anapatia mafunzo maafisa mbali mbali nchini Malawi kuzuia na kukabili uhalifu: mwaka huu pekee licha ya janga la Corona au COVID-19, ameweza kuokoa watu 300 waliokuwa wakumbwa na usafirishaji haramu sambamba na kukamata watu 31 wahusika wa uhalifu huo.