
Umuhimu wa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa katika wakati huu wa janga la Corona
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa limechukua jukumu muhimu katika kukabiliana na janga la COVID-19, tangu mgonjwa wa kwanza alipotangazwa katika mji wa China, Wuhan mnamo mwezi Desemba mwaka jana 2019. Kwenye mkutano na waandishi wa habari mkuu wa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, anazitaja sababu tano za umuhimu wa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa katika wakati huu wa Janga la Corona kuwa ni:
1) Kusaidia nchi kujiandaa na kutoa mwelekeo
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limetoa wito wa utayarishaji wa mpango na mpangilio wa kukabiliana na COVID-19, ambao unaashiria hatua kuu ambazo nchi zinahitaji kuchukua, na rasilimali zinazohitajika.
Ofisi sita za wakala wa afya, na ofisi za nchi 150, zinashirikiana kwa karibu na serikali ulimwenguni kuandaa mifumo yao ya kiafya kwa mujibu wa COVID-19, na kutoa msaada unaofaa wakati wagonjwa wanaporipotiwa na pia visa vinapoanza kuongezeka.

Na washirika wa WHO walianzisha mfuko wa mwelekeo na mshikamano wa COVID-19, ili kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma wanazohitaji, na wafanyikazi wa mstari wa mbele wanapata vifaa na taarifa muhimu; na kuharakisha utafiti na ukuzaji wa chanjo na matibabu kwa wote wanaohitaji.
“Hivi sasa tumepata michango kutoka kwa serikali, sekta binafsi na watu binafsi, zaidi ya dola milioni 800 zimeahidiwa na kuendelea kupokelewa.” Anasema Dkt Tedros.
2) Kupeana habari sahihi, na kutupilia mbali habari za kupotosha
Mtandao una habari tofauti na za kupotosha kuhusu janga hili, habari zingine zinafaa, zingine ni za uwongo au za kupotosha. WHO ina mwongozo sahihi na mzuri ambao unaweza kusaidia kuokoa maisha. Ili kuhakikisha kuwa habari wanazopata watu ni sahihi na zinasaidia, Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO lilianzisha timu inayosaidia kwa kuwapa watu ushauri ulio sahihi na rahisi kuelewa. WHO ina wataalamu wa afya na wanasayansi, pamoja na wataalam wa magonjwa ya kila aina na wanasayansi hodari, ili kuhakikisha kuwa wanafanya kazi iliyo safi na kupeana mwelekeo unaofaa kwa njia zote wanafanya ripoti za matokeo ya kila siku na muhtasari wa waandishi wa habari, pamoja na maelezo mafupi yalio fanyika na serikali,kuhakikisha kila mtu duniani anapata ujumbe muhimu kuhusiana na mlipuko huu.

Vyombo vingi vya habari vya kijamii na teknolojia vinafanya kazi kwa karibu na Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kusaidia kuenea wa habari za uhakika, pamoja na Instagram, Linkedin na TikTok; na mazungumzo kwenye mitandao ya whatsapp na Viber yamepata mamilioni ya wafuasi, kutuma habari na ripoti kwa wakati unaofaa.
3. Kuhakikisha vifaa muhimu vinawafikia wafanyikazi wa afya walio kwenye mstari wa mbele katika janga hili.
Vifaa vya kinga ya kibinafsi ni muhimu kuhakikisha wataalamu wa afya wana uwezo wa kuokoa maisha yaw engine nay a kwao. Kufikia sasa, WHO imesafirisha zaidi ya vifaa milioni mbili vya kinga binafsi kwa nchi 133, na inajiandaa kusafirisha vitu vingine milioni mbili katika wiki zijazo. Vipimo zaidi ya milioni vya utambuzi vimetumwa kwa nchi 126.

Lakini zaidi WHO inafanya kazi na wadau mbalimbali na wengine katika sekta binafsi, kuendeleza utengenezaji na usambazaji wa vifaa muhimu vya matibabu.
Mnamo tarehe 8 Aprili, WHO ilizindua Kikosi kazi cha usambazaji ambacho kinasadia kuongeza kwa haraka vifaa muhimu vya kinga mahali vinakohitajika.
4) Kufundisha na kuhamasisha wafanyikazi wa afya
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linakusudia kutoa mafunzo kwa mamilioni ya wafanyakazi wa afya, kupitia jukwaa lake la OpenWHO. Shukrani kwa zana hii ya mtandao, maarifa ya kuokoa maisha huhamasishwa kwa wafanyakazi wa mstari wa mbele.

OpenWHO pia inafanya kazi kwa njia ya kushiriki kugawana utaalam wa afya ya umma, na majadiliano ya kina na maoni juu ya masuala muhimu. Kufikia sasa, zaidi ya watu milioni 1.2 wamejiandikisha katika lugha 43.

Nchi pia zinaungwa mkono na wataalam kote ulimwenguni na Mtandao Global Outbreak Alert and Response Network (GOARN). Wakati wa milipuko, mtandao huhakikisha kuwa utaalamu na ustadi sahihi wa ufundi unafanya kazi wakati unahitajika sana.
Timu za Dharura za matibabu ya dharura pia ni sehemu muhimu ya wafanyikazi wa afya duniani. Timu hizi zinapata mafunzo mengi sana, na zinajitosheleza, na hutumwa kwa maeneo yaliyoainishwa kama maeneo ya maafa au ya dharura.
5) Kutafuta chanjo
Maabara katika nchi nyingi tayari zinafanya majaribio ambayo, yanatarajiwa, mwishowe yatasaidia kwa chanjo. Katika jaribio la kujaribu juhudi hizi, Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO lilileta pamoja watafiti 400 wakuu wa ulimwengu mnamo mwezi Februari, ili kubaini na kusaidia kupata suluhu.