Rushwa na jinsia

21 Januari 2020

Wanawake na wanaume wanathirika tofauti na rushwa au ufisadi, lakini hakuna ushahidi wa kubainisha nani kati yao anaathirika kidogo.

Rushwa huathiri vibaya idadi ya watu walio katika mazingira yaliyo hatarini na huwakumba maskini zaidi, haswa wanawake, ambao wanawakilisha idadi kubwa ya maskini ulimwenguni.

Katika jamii, jinsia kawaida huamua mgawanyiko wa kazi, udhibiti wa rasilimali na uamuzi, kutoka kwenye ngazi ya mashinani hadi ngazi ya serikali.

Ingawa masomo kadhaa ya kitaaluma yameonyesha uhusiano fulani kati ya idadi ya wanawake katika ngazi ya maamuzi na ushawishi na hatua dhidi ya rushwa, haimaanishi kwamba ni kweli kiwango cha juu cha ushiriki wa wanawake katika maisha ya jamii kingesadia viwango vya ufisadi kuwa vya chini.

Ili kuhakikisha kuwa uundaji wa sera umezingatia takwimu, utafiti zaidi unahitajika. Hakuna uthibitisho kamili, kwa mfano, kwamba wanawake ni mafisadi zaidi au la kuliko wanaume.

Bango lenye ujumbe wa ufisadi nchini Namibia
Bank ya Dunia/Philip Schuler
Bango lenye ujumbe wa ufisadi nchini Namibia

Ufisadi unaathirije tofauti wanawake?

Majukumu ya kijinsia na mitindo pia vinaweza kuathiri vibaya wanawake hivyo kuwasababisha kulipa  hongo zaidi ili kupata huduma za umma na kwa hivyo kukiuka haki za binadamu.

Ambapo wanawake wanabaki kuwa watunzaji wa msingi wa familia, wanaweza kukumbana na rushwa wanapopata huduma za umma za msingi kama vile afya, elimu, maji na usafi. Wanalazimika kulipa rushwa ili kupata huduma za msingi ambazo zinaweza kuwa asilimia kubwa ya mapato yao ikilinganishwa na wanaume, hivo kusababisha mzunguko mbaya wa umaskini.

Kuna ushahidi pia kwamba utumiaji wa mwili wa binadamu, kingono au vinginevyo, unaweza kutumika kama sarafu katika ufisadi.

Hitaji la wanawake la huduma za afya ya uzazi linaweza kuwaweka kweney hatari ya watoa huduma za afya wafisadi.

Watoto wanaweza kunyimwa elimu kabisa wakati familia haziwezi kumudu gharama za masomo ambazo zinaweza kuongezeka kupitia mahitaji ya rushwa.

Wanawake mashinani waliweka biashara na ajira kama eneo la pili la juu la huduma inayathirika na hongo baada ya sekta za umma.

Vikundi vilivyo hatarini katika jamii mara nyingi vinakabiliwa na rushwa ya pesa au huombwa huduma za kingono ili wapate ajira au kufanya biashara, na hii inasababisha kuzuia uwezo wao wa kupata mapato au kuendeleza biashara zao.

Ubadilishanaji wa fedha.
UNDP Ukraine
Ubadilishanaji wa fedha.

 

Je, wanawake ni mafisadi zaidi kuliko wanaume?

UNODC tayari inatoa orodha kamili ya programu zinazopambana na rushwa na sasa inachunguza jinsi mwelekeo wa kijinsia unavyoweza kuingizwa katika programu zilizopo pamoja na programu mpya za kuongeza ufanisi na uendelevu wao na kuhakikisha kuwa shughuli zinaundwa ili kuwanufaisha wanaume na wanawake sawa.

Mpango wa Elimu kwa ajili ya haki (E4J) umeunda kitengo cha chuo kikuu kuhusu viwango vya maadili ya kijinsia na unaendeleza masuala kuhusu jinsia na ufisadi

Mkutano ulioandaliwa na UNODC wa wataalam 26 kutoka kwenye asasi za kiraia, mamlaka za kitaifa za kupambana na rushwa, mashirika ya kimataifa na wanazuoni mjini Bangkok mnamo Septemba 2018, ulitathmini maarifa yaliyopo na uelewa wa jinsia na rushwa na wataalam walipendekeza suluhisho na kubaini mazoea mazuri.

Wataalam walikubaliana kuhusu mapendekezo ya hatua katika maeneo manne: uadilifu wa haki za jinai, sekta binafsi, ushiriki wa mashirika ya umma na huduma za umma.

Mazungumzo hayo yaliweka misingi ya utafiti uliofanywa na UNODC kuongeza majadiliano na kuchunguza zaidi uhusiano kati ya jinsia na ufisadi ambao utachapishwa mwaka huu wa 2020.

Kandoni mwa Mkutano wa kimataifa mjini Abu Dhabi, kwa mara ya kwanza kulikuwa na hafla maalum juu ya mada iitwayo "Kuchunguza mipaka ya jinsia ya ufisadi", uliofanyika Alhamisi ya tarehe 19 Desemba mwaka 2019.

Walioshiriki ni pamoja na Jumuiya ya Kimataifa ya majaji Wanawake, Transparency Maroc, Tume ya Haki za Binadamu na Haki ya Utawala ya Ghana, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo (UNDP) na UNODC.

Wakati ngazi za juu za ushiriki wa wanawake katika mamlaka unahusishwa na utawala bora na viwango vya chini vya ufisadi katika nchi nyingi, si sahihi kuhitimisha kuwa kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi za maamuzi kutapunguza rushwa moja kwa moja.

Kuzingatia uwezeshaji wa wanawake kunapaswa kuwa sehemu muhimu ya ajenda ya kupambana na ufisadi kwani wanawake wanaweza kuwa mawakala chanya wa mabadiliko katika kukabiliana na jinamizi la rushwa na kutumia vipimo vya jinsia vya vita dhidi ya rushwa kunaweza kusababisha jamii zenye umoja na ushirikiano zaidi.

Utafiti zaidi unahitajika kuangalia tofauti ya jinsi watu wanavyokabiliana na rushwa na jinsi mipango ya kupambana na rushwa inavyowaathiri wanawake na wanaume.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter