Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA: Maeneo Saba ambayo AI itabadilisha Sayansi na Teknolojia

Michoro ya sanaa inayoonyesha matumizi ya akili ya bandia.
© IAEA/А. Варгас
Michoro ya sanaa inayoonyesha matumizi ya akili ya bandia.

IAEA: Maeneo Saba ambayo AI itabadilisha Sayansi na Teknolojia

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katika muongo mmoja uliopita, teknolojia zinazohusiana na akili mnemba maarufu kama AI zimekua upesi zaidi na  zenye uwezo wa kutatua matatizo yanayozidi kuwa magumu. Akili mnemba inatumika katika sekta mbalimbali, kama vile viwanda, usafirishaji, fedha, elimu, na afya. Vile vile, akili mnemba inaweza kuchangia maendeleo ya sayansi ya nyuklia, teknolojia na matumizi yake. Kutumia nguvu za akili mnemba katika uwanja wa nyuklia kunaweza kutoa mchango mkubwa katika kutatua changamoto kubwa zaidi za wakati wetu, kutoka kwa kupambana na mabadiliko ya tabianchi hadi kuhakikisha kuna uhakika wa chakula.

Yafuatayo ni maeneo machache ambapo akili mnemba inaweza kuwa na manufaa katika matumizi yenye amani ya teknolojia ya nyuklia kwa sasa na siku zijazo  kama ilivyochapishwa kwneye wavuti wa IAEAAkili Mnemba Kuharakisha Matumizi ya Teknolojia ya Nyuklia, Sayansi na Teknolojia .

Mtaalamu wa Sri Lanka, aliyefunzwa katika maabara za IAEA huko Seibersdorf, Austria, akiangalia kipimo cha iodini-131 kitakachotolewa kwa wagonjwa wa saratani ya tezi dume katika Kitengo cha Dawa ya Nyuklia huko Peradeniya, Sri Lanka. Picha: IAEA
IAEA
Mtaalamu wa Sri Lanka, aliyefunzwa katika maabara za IAEA huko Seibersdorf, Austria, akiangalia kipimo cha iodini-131 kitakachotolewa kwa wagonjwa wa saratani ya tezi dume katika Kitengo cha Dawa ya Nyuklia huko Peradeniya, Sri Lanka. Picha: IAEA

1.      Afya ya binadamu

Akili mnemba inaweza kusaidia kutibu magonjwa mbalimbali. Tayari inatumika katika utambuzi na matibabu ya saratani: shukrani kwa uboreshaji wa usindikaji wa picha na ufafanuzi sahihi wa uvimbe. Akili mnemba inawezesha  maendeleo katika  upangaji mwafaka zaidi wa matibabu na tiba ya mionzi ilio na uwezo wa kubadilika, yaani, matibabu yanayolingana na hali ya mwili wa mgonjwa fulani. Matumizi ya teknolojia ya akili mnemba kwa matibabu ya saratani yanafanyiwa utafiti katika nchi nyingi duniani, zikiwemo China, Urusi, Uingereza, Marekani na Ufaransa. Hivi karibuni IAEA ilizindua mradi wa utafiti ulioratibiwa katika eneo hili.

Akili mnemba pia itakuwa na jukumu muhimu katika mpango wa IAEA wa Zoonotic Disease Integrated Action (ZODIAC), ambao unalenga kusaidia wataalam kuelewa vyema athari za magonjwa ya zoonotic kwa afya ya binadamu, pamoja na kutabiri, kutathmini na kuthibiti milipuko ya baadaye ya magonjwa ya zoonotic.

2.      Chakula na kilimo

Matumizi ya AI, pamoja na teknolojia ya nyuklia, yanaweza kusaidia kuboresha ustahimilivu wa mifumo ya chakula na ustahimilivu wao dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, na pia kuthibiti uhakika wa upatikanaji wa chakula.

Wataalamu wanatumia akili mnemba kuchakata na kuchambua takwimu ili kuongeza mavuno ya mazao, kutathmini unyevu wa udongo, kuboresha mifumo ya umwagiliaji, kugundua na kutabiri ulaghai wa chakula, na kurejesha ardhi iliyochafuliwa na vitu vyenye mionzi.

Mboga yakiuzwa katika soko dogo la ndani katika kijiji cha Doi Son, Mkoa wa Ha Nam, Vietnam.
© WHO/Quinn Mattingly
Mboga yakiuzwa katika soko dogo la ndani katika kijiji cha Doi Son, Mkoa wa Ha Nam, Vietnam.

3. Maji na mazingira

Mbinu za Isotopiki huruhusu wataalam kuutafiti na kufuatilia mwendo wa maji katika hatua tofauti za mzunguko wake, pamoja na mabadiliko katika mzunguko huo yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Wataalamu tayari wanatumia mbinu zenye msingi wa akili mnemba kuchambua kwa haraka kiasi kikubwa takwimu za kisitopiki zinazohusiana na maji zilizohifadhiwa katika hifadhidata za kimataifa, kama vile Muungano wa Kimataifa wa Kunyesha kwa Isotopu, GNIP unaodumishwa na IAEA na Shirika la Hali ya Hewa Duniani.

Uchanganuzi bora na wenye ufanisi wa takwimu kwa kutumia akili mnemba huwasaidia wanasayansi kuelewa vyema michakato ya mabadiliko ya tabianchi na athari zake katika upatikanaji wa maji duniani kote.

4. Utafiti wa Sayansi na mchanganyiko wa Nyuklia

Akili mnemba inachukua jukumu muhimu zaidi katika sayansi ya nyuklia. Inatumika kwa uchanganuzi wa data, uundaji wa kinadharia, na majaribio, mambo ambayo yanasaidia kukuza uvumbuzi wa kiteknolojia na kuharakisha utafiti wa kimsingi, kama vile katika ukusanyaji na uchanganuzi wa takwimu za nyuklia na zile za atomiki.

Utafiti wa mchanganyiko au Fusion ndio eneo ambalo matumizi ya akili mnemba yana faida zaidi. Kwa uwezo wake wa kutatua matatizo makubwa na yenye utata, akili mnemba huenda ikawezesha majaribio na uvumbuzi wa kisayansi kwa njia ya uundaji na uigaji. Programu hizi za akili mnemba zimejumuishwa katika mradi mpya wa utafiti wa miaka mitano ulioratibiwa na IAEA, unaolenga kuharakisha utafiti na maendeleo ya mchanganyiko.

Ndani ya mnara wa kupoeza kwenye Kiwanda cha Nguvu za Nyuklia cha Chernobyl kaskazini mwa Ukrainia.
© Unsplash/Mick De Paola
Ndani ya mnara wa kupoeza kwenye Kiwanda cha Nguvu za Nyuklia cha Chernobyl kaskazini mwa Ukrainia.

5. Nishati ya nyuklia

Nishati ya nyuklia, ambayo ni chanzo cha kuaminika cha nishati yenye kiwango cha chini cha kaboni, inaweza kufaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na akili mnemba. Kwa kuchanganya uigaji wa kidijitali wa mitambo halisi ya nyuklia  na mifumo ya akili mnemba, taratibu changamano katika tasnia ya nyuklia zinaweza kuboreshwa na muundo wa mtambo, utendakazi na usalama wake kuboreshwa. Uboreshaji kama huu unaweza kuongeza ufanisi wa kazi na kupunguza gharama za utunzaji.

Mafunzo ya mashine, namna ambayo ambao akili mnemba hujifunzia kwa kuchanganua kiasi kikubwa cha takwimu, husaidia kufanya kazi kiotomatiki, na hivyo kuongeza kutegemewa na kupunguza uwezekano wa makosa. Kadhalika, akili mnemba ina uwezo mkubwa wa uchambuzi na utabiri wa kufuatilia michakato katika mitambo ya umeme na kutambua hitilafu.

Takwimu za 2021 zilizowasilishwa wakati wa mkutano wa mtandaoni wa AI for Nuclear Power zinaangazia uwezo wa akili mnemba katika kupunguza gharama za uendeshaji na utunzaji wa mitambo  ya nyuklia. Kuzimwa kwa ghafla kwa jenereta iendeshwayo na magurudumu ya upepo ya turbine kwenye kiwanda cha nguvu za nyuklia nchini Urusi hugharimu mwendeshaji wastani wa Euro milioni moja kwa siku. Badala yake, udhibiti wa ubashiri unaoendeshwa na akili mnemba unaweza kusaidia kuratibu uzimaji wa viwanda hivi na kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama na idadi ya kuzimwa bila kupangwa.

6. Usalama wa Nyuklia na Ulinzi dhidi ya Mionzi

Huku nchi nyingi zikitumia teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani na kutekeleza programu za nishati ya nyuklia, IAEA inafanya kazi kila mara kulinda watu na mazingira kutokana na mathara ya mionzi ya chuma.

Akili mnemba inaweza kuwa muhimu katika kuhakikisha usalama na ulinzi wakati tunapotumia nyuklia. Inaweza kutumika katika kuchakata takwimu zinazotoka kwenye  mifumo ya ufuatiliaji wa mionzi ili kuboresha utambuzi wa nyuklia na vifaa vingine vinavyotumia mionzi. Akili mnemba pia inaweza kutumika kuchanganua takwimu kutoka kwa mifumo ya ulinzi halisia na kugundua wapenyezaji au hitilafu ambazo zinaweza kuashiria shambulio la mtandao kwenye kituo cha nyuklia. Vilevile, ujumuishaji wa akili mnemba katika programu zinazohusiana na viwango vya usalama dhidi ya mionzi unaweza kusaidia kuboresha kiwango cha ulinzi kwa mamilioni ya wafanyakazi wanaokabiliwa na mionzi wawapo kazini katika taaluma za uuguzi, ujenzi, madini, usafirishaji, kilimo na nguvu za nyuklia.

Akili Mnemba inaweza kuchangia katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na kusaidia maendeleo kuelekea SDGs zote.
UN Photo/Elma Okic
Akili Mnemba inaweza kuchangia katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na kusaidia maendeleo kuelekea SDGs zote.

7. Ulinzi wa nyuklia

Ulinzi ni hatua za uthibitishaji wa kiufundi ambapo IAEA hutoa ushahidi wa kuaminika kwamba nchi zimetimiza wajibu wao wa kisheria wa kutumia nyenzo za nyuklia kwa madhumuni ya amani pekee. Kupitia hatua kama vile ukaguzi wa vifaa, hasa vifaa vya nyuklia, IAEA inachambua nyenzo na shughuli za nyuklia zilizoidhinishwa kimataifa ili kubaini shughuli ambazo hazijaidhinishwa.

Ulinzi wa IAEA unatokana na kiasi kikubwa cha takwimu zilizopatikana kwa njia mbalimbali, kama vile picha za setilaiti, sampuli za mazingira, uchunguzi wa mionzi ya gamma na ufuatiliaji wa video. Akili mnemba  inaweza kusaidia IAEA kulinda wakaguzi na wachambuzi katika kuchanganua takwimu hizi. Mbinu za kujifunza kupitia mashine tayari zinatumika kuchanganua kiasi kikubwa cha takwimu ili kubaini uzalishaji na kusaidia katika uthibitishaji wa mafuta na video za ufuatiliaji zilizotumika. Akili mnemba inatarajiwa kuboresha zaidi ufanisi na kutegemewa kwa uhakikisho kwa kupunguza idadi ya kazi za kurudia-rudia zinazofanywa na wakaguzi.