Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kusini Mashariki mwa Asia vyumba vya utesaji na baa vyahusika na uhalifu wa kupangwa: UNODC

Malaghai ambaohawatimizi kiwango wanachotakiwa huteswa
UNODC/Laura Gil
Malaghai ambaohawatimizi kiwango wanachotakiwa huteswa

Kusini Mashariki mwa Asia vyumba vya utesaji na baa vyahusika na uhalifu wa kupangwa: UNODC

Na  Daniel Dickinson and Jessica Jiji nchini Ufilipino
Sheria na Kuzuia Uhalifu

Makundi ya uhalifu wa kimataifa yaliyoko Kusini-mashariki mwa Asia yanachochea usafirishaji haramu wa watu, ama kwa kuwalazimisha kufanya uhalifu au unyonyaji wa kingono katika kile kinachoitwa "mitandao ya kitapeli" ambayo imeenea katika eneo lote, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Inakadiriwa kuwa kuna makundi 400 hivi ya uhalifu nchini Ufilipino pekee. Takriban kila mara huendeshwa kwa siri na kinyume cha sheria pamoja na shughuli zilizoidhinishwa na halali za michezo ya bahatinasibu mtandaoni.

Kuongezeka kwa makundi ya ulaghai mtandaoni yanayolenga waathiriwa kote ulimwenguni ni jambo jipya ambalo lililipuka wakati wa janga la coronavirus">COVID-19.

Tume ya Rais ya Ufilipino ya Kupambana na Uhalifu wa Kupangwa  (PAOCC) imevamia na kuzima makumi ya operesheni katika miaka ya hivi karibuni na inashirikiana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu UNODC, kuangalia njia za kufanya kazi na nchi zingine kuvuruga na kusambaratisha magenge hayo ya kashfa katika nchi za Kusini-mashariki mwa Asia, ikiwa ni pamoja na Ufilipino, Cambodia, Laos na Myanmar.

Kituo cha  ulaghai kama hiki kilicho Kaskazini mwa mji mkuu wa Ufilipino Manila kinahifadhi mamia ya wafanyakazi
UN News/Daniel Dickinson
Kituo cha ulaghai kama hiki kilicho Kaskazini mwa mji mkuu wa Ufilipino Manila kinahifadhi mamia ya wafanyakazi

Daniel Dickinson wa UN News alitembelea maeneo mawili yaliyovamiwa katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila, na Bamban kaskazini. Alizungumza na watu wawili: Susan, Mfilipino na Dylan* kutoka Malaysia ambao walilazimishwa kutekeleza ulaghai. Pia alikutana na Winston Casio wa PAOCC.

Susan: Dada yangu wa kambo alinidanganya niondoke nyumbani na kusafiri hadi Myanmar ambako niliahidiwa kazi ya uuzaji katika kampuni yake. Ikawa kituo cha utapeli, na nililazimika kufanya kazi ili kulipa madeni ya dada yangu kwa vile alikuwa amekimbia.

Nilitengeneza wasifu wa uwongo, kama mwanamke kijana tajiri aliyeishi Brooklyn, New York, ambaye alikuwa na mali na biashara. Wasimamizi walinipa picha kutoka kwa akaunti ya Instagram ili kumjenga mhusika na kuniambia niwasiliane na wanaume waliotalikiana au wapweke huko Merikani ili wanitumie pesa. Hii ndio inaitwa "kashfa au ulaghai wa mapenzi". Katika picha, tabia yangu ni ununuzi daima. Lakini sikuweza hata kwenda nje. Nilinaswa ndani ya jengo hilo.

Tunapewa hati za kutumia katika mazungumzo ya maandishi, na waliponiambia niboreshe, nilitumia programu ya apu ya sarufi kuangalia Kiingereza changu. Ikiwa mteja anataka kukutana nawe kwa njia ya Video, wana wanamitindo wanaotekeleza jukumu hilo. Ambao pia walisafirishwa kiharamu.

Susan alisafirishwa kiharamu hadi kwenye kituocha utapeli Myanmar
UNODC/Laura Gil
Susan alisafirishwa kiharamu hadi kwenye kituocha utapeli Myanmar

Dylan: Watu wengi hawachagui kuwepo hapo. Lazima ufanye kazi hadi saa 16 kwa siku, haswa kwani lazima uwasiliane na wateja katika saa za maeneo yao. Wasimamizi waliniambia niwafanye wawekeze kwenye dili hewa za mafuta huko Dubai kisha waibe pesa zao.

Kuna sehemu za kiasi cha pesa ambazo lazima utapeli. Waliniwekea lengo la kiwango cha dola 100,000 kwa mwezi, na nilipokosa  kufikisha, nilipigwa.

Winston Casio: Tuliokoa takriban watu 680 katika kituo cha ulaghai cha Bamban, lakini tunadhani kuwa baadhi ya wasimamizi walitoroka baada ya kufahamishwa.

Hizi ni shughuli kubwa. Watu hawaruhusiwi kuondoka. Wanashikiliwa kinyume na matakwa yao na kulazimishwa kufanya ulaghai na utapeli. Wanawake wanauzwa kama watumwa wa ngono, na wasimamizi katika kituo kimoja walikuwa na kile walichokiita "aquarium" ambapo wanawake walinadiwa kwa nguvu na kisha kuchaguliwa na wanaume kufanya ngono.

Winston Casio akiwa amesismama kwenye duka la kinyozi katika kituo cha utapeli cha Manila
UN News/Daniel Dickinson
Winston Casio akiwa amesismama kwenye duka la kinyozi katika kituo cha utapeli cha Manila

Kila eneo linajitegemea, na kila kitu mnapewa. Kwa kweli, kuna mabweni na mikahawa, lakini pia duka la kinyozi, kliniki ya matibabu, spa ya massage, chumba cha kucheza kamari na baa ya kuimba karaoke ya watu mashuhuri VIP kwa ajili ya wasimamizi wakuu, ambapo wanaweza kunywa, kuimba na kuburudika katika vyumba vya binafsi.

Mita chache tu kwenye ushoroba wa ukumbi, pia tulipata chumba cha mateso na pingu na damu kwenye kuta, ambapo watu walichukuliwa kwa adhabu ya kikatili wakati hawakufikia kiwango chao cha fedha.

Katika kituo kimoja tulichovamia, kulikuwa na wanaume wawili waliokuwa na hati za kusafiria za Rwanda ambao walijulikana kama watekelezaji sheria, ambao kazi yao ilikuwa ni kuvuta watu kutoka kwenye madawati au vitanda vyao usiku ili kuwapiga.

Susan: Nilikaribia kuwalaghai baadhi ya wateja lakini nilijisikia vibaya kuhusu hilo hivyo nikawaonya kwa siri huku nikimwambia meneja wangu kwamba walikuwa wamenizuia. Alikasirika na kunipiga kwa bomba la chuma. Majeraha yangu yalikuwa makubwa sana kuweza kutibiwa kwenye kituo cha utapeli, kwa hiyo nilipelekwa hospitalini na walinzi watatu lakini sikuweza kuwaeleza madaktari kilichonipata. Bado ninateseka kimwili na kihisia-moyoni

Baa ya watu mashuhuri ilikuwa kifanyakazi mita chache tu kutokaushoroba wa  chumba cha mateso
UN News/Daniel Dickinson
Baa ya watu mashuhuri ilikuwa kifanyakazi mita chache tu kutokaushoroba wa chumba cha mateso

Dylan: Sikupata mshahara wowote lakini nilianza kujiongezea deni kwani nililazimika kulipia chakula, ambacho kiligharimu mara mbili hadi tatu zaidi kwenye kituo hicho cha utapeli kuliko nje. Niliachiliwa baada ya mwezi mmoja kituo kilipovamiwa.

Makaratasi ya maelezo yaliyokuwa yakitumiwa na wafanyakazi kuaghai  watu yakiwa yametandazwa mezani baada ya polisi kuvamia kituo hicho
UNODC/Laura Gil
Makaratasi ya maelezo yaliyokuwa yakitumiwa na wafanyakazi kuaghai watu yakiwa yametandazwa mezani baada ya polisi kuvamia kituo hicho

Winston Casio: Wakati mwingine ni vigumu kujua tofauti kati ya waathiriwa na walaghai. Kuna matukio ambapo watu huchukuliwa kinyume na mapenzi yao, lakini ambao baada ya mafunzo ya siku nne hadi tano, kukumbatia shughuli haramu na kustawi na kwa kweli kupata pesa. Sheria inataka kuona hali hii katika rangi nyeusi na nyeupe, lakini kuna maeneo mengi ya kijivu.

Ni jambo la kustaajabisha kusema kwamba hali hii ina changamoto, kwani mitandao ya kimataifa ya uhalifu iliyopangwa ambayo inaendesha vituo hivi huwa iko hatua tatu au nne mbele yetu.

Hili ni tatizo la kikanda ambalo hakuna nchi moja inayoweza kulitatua. Huu ni uhalifu uliopangwa. Susan atathibitisha kuwa samani na vifaa vya kompyuta ni sawa katika vituo vya Myanmar na Ufilipino.

Mashirika ya kutekeleza sheria kote Kusini-mashariki mwa Asia yanahitaji kushirikiana na kuratibu, na hii ndiyo sababu UNODC ni muhimu. Inaweza kuleta nchi pamoja na kutoa utaalamu, kwa mfano, katika uchunguzi wa kisayansi wa kidijitali.

Kituo cha kazi ya ulaghai kilitelekezwa baada ya kuvamiwa na polisi Manila
UN News/Daniel Dickinson
Kituo cha kazi ya ulaghai kilitelekezwa baada ya kuvamiwa na polisi Manila

Susan: Kuelekea mwisho, nilipigwa mara 13 kwa siku moja. Niliomba tu na kuomba huku wakinipiga. Nililazimika kuwapigia simu wazazi wangu na kuwaomba walipe dola 7,000 kwa ajili ya fidia yangu, ambayo ilikuwa gharama ya bili ya hospitali. Hawakuwa na pesa, na nikawaambia wasijaribu kuzilipa. Niliwaambia wasimamizi wangu ‘niueni tu.’

Hawajali watu. Wanajali pesa tu. Hata hivyo, mwishowe waligundua kwamba sikuwa na pesa na kwamba sikuwa na manufaa yoyote, hivyo wakaniacha tu. Nilipitia Thailand hadi Ufilipino.

***

Susan sasa anafanya kazi PAOCC huko Manila, na Dylan amekubali kuwa shahidi katika hatua zinazowezekana za kisheria zinazokuja na anatumai hatimaye kurejea nyumbani kwake Malaysia.

*Hayo sio majina yao halisi

TAGS: Uhalifu wa kupangwa, utapeli, ulaghai, Ufilipino, Myanmar, UNODC