Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaimarisha sekta ya kakao Côte d'Ivoire kupambana na mabadiliko ya tabianchi

Wazalishaji wa kakao nchini Côte d'Ivoire wamekabiliwa na changamoto zinazoongezeka za hali ya hewa, kwani zao la kakao ni nyeti sana kwa mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa usaidizi kutoka kwa FAO na Mfuko wa Hali ya Hewa ya Kijani, wamepitisha mbinu za kil…
©FAO/Amanda Bradley
Wazalishaji wa kakao nchini Côte d'Ivoire wamekabiliwa na changamoto zinazoongezeka za hali ya hewa, kwani zao la kakao ni nyeti sana kwa mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa usaidizi kutoka kwa FAO na Mfuko wa Hali ya Hewa ya Kijani, wamepitisha mbinu za kilimo mseto, na kufanya mazao hayo kustahimili zaidi na kuongeza mavuno.

FAO yaimarisha sekta ya kakao Côte d'Ivoire kupambana na mabadiliko ya tabianchi

Tabianchi na mazingira

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, miti ya kakao katika shamba la Monique N'Guessan Amlan mashariki mwa Côte d'Ivoire imekuwa ikistawi vizuri.

Hii ni tofauti na hapo awali, ambapo miti mingine ilikuwa inakauka na kufa kabisa kutokana na jua kali la kitropiki, hali iliyomfanya mjane Monique huyu mwenye umri wa miaka 64 nchini humo kushindwa kuwasaidia watoto wake wanne ambao bado wanaendelea na masomo yao.

“Nimeona kwamba miti ya kakao inakua vizuri,  na mavuno kutoka kwenye shamba langu yameongezeka sana,” anasema Monique. Mavuno yake yameongezeka kutoka kati ya kilo 120-150 kwa ekari hadi zaidi ya kilo 250 kwa ekari. Na hii, si tu kutokana na idadi ya kakao iliyoboreshwa bali pia ubora na uendelevu wa mazingira, ambayo  ni habari njema kwa sababu, kama anavyosema, “Wanunuzi wa kimataifa wanatilia mkazo mkubwa uendelevu wa mbinu za kilimo.”

Miti ya kakao ya Monique imeharibika zaidi ya miaka miwili iliyopita, na mavuno yakiongezeka kutoka kati ya kilo 120-150 kwa hekta hadi zaidi ya kilo 250 kwa hekta.
©FAO/Mino Randrianarison.
Miti ya kakao ya Monique imeharibika zaidi ya miaka miwili iliyopita, na mavuno yakiongezeka kutoka kati ya kilo 120-150 kwa hekta hadi zaidi ya kilo 250 kwa hekta.

Monique alianza kuona mabadiliko haya baada ya kujisajili kwenye mradi unaotekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO na kufadhiliwa na Mfuko wa kijamii unaojali mazingira GCF.

Kwa ushirikiano  na Serikali ya Côte d'Ivoire, mradi unawafundisha wakulima wa kakao mbinu za kilimo cha uingizaji wa miti na vichaka katika mifumo ya kilimo badala ya kilimo cha kakao cha jadi ambacho mara nyingi kinahusisha ukataji wa miti. Mradi huo unaoitwa PROMIRE, au Kukuza Uzalishaji wa Kakao Usio na Ukataji wa Miti ili Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ukaa, unalenga kujenga mnepo  dhidi ya mabadiliko ya tabianchi  na kupunguza gesi chafuzi katika mnyororo wa uzalishaji wa kakao wa Côte d'Ivoire

Chini ya mradi huu wa FAO, Monique alipokea miti ya matunda kadhaa na aina nyingine za mimea ya kupanda pamoja na miti ya kakao, ili kuongeza kivuli zaidi. Pia alipewa kifaa cha kumsaidia katika kupogoa vizuri, kuondoa maji na kuvuna.

Miti ya kakao ya Monique imeharibika zaidi ya miaka miwili iliyopita, lakini kwa sasa mavuno yameongezeka kutoka kati ya kilo 120-150 kwa hekta hadi zaidi ya kilo 250 kwa hekta.
©FAO/Amanda Bradley
Miti ya kakao ya Monique imeharibika zaidi ya miaka miwili iliyopita, lakini kwa sasa mavuno yameongezeka kutoka kati ya kilo 120-150 kwa hekta hadi zaidi ya kilo 250 kwa hekta.

Mimea ya kakao na mazao ya kakao huathiriwa sana na mabadiliko ya hali ya hewa kama vile kuongezeka kwa joto na mifumo isiyotabirika ya mvua inayotokana na mabadiliko ya tabianchi. Maeneo makuu ya uzalishaji wa kakao nchini humo tayari yameathiriwa na mvua kubwa na mafuriko, na hofu ya kupungua kwa ugavi wa kakao imefanya bei yake kupanda hadi viwango vya juu, ikiongezeka kwa asilimia 136 kati ya Julai 2022 na Februari 2024, huku thamani ya hisa za kakao ikifikia dola 10,000 kwa mara ya kwanza.

Monique anasema aliposikia mara ya kwanza kuhusu mradi wa PROMIRE, hakuwa na uhakika kama ungeweza kumsaidia sana. Kifo cha mumewe karibu miaka 20 iliyopita kilimuacha si tu na pengo la kihisia, bali pia upungufu wa rasilimali zinazohitajika kulima shamba lake la kakao lenye ukubwa wa ekari moja na kuisaidia familia yake.

Lakini sasa, anasema, “Msaada ninaopata unaiimarisha imani yangu kuwa mabadiliko yanawezekana. Nikifaulu kuishi maisha marefu, najua nitafurahia manufaa ya miti ninayopanda sasa.”

Monique anatarajia kutoa ufahamu wa changamoto zinazowakabili, hasa kwa wazalishaji wa kakao wajane kama yeye, na kuwahimiza kujiunga na mradi akisema “ili tuweze kuunda mazingira ya haki kwa wakulima wa kiume na wa kike, na kuhakikisha mustakabali endelevu kwa familia zetu na jamii zetu.”

Kwa mujibu wa FAO mradi huu sio tu unahusu kukabiliana na ukataji wa miti na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa miti ya kakao, bali pia ni wa kusaidia wakulima wa kiume na wa kike kuwa na ujuzi zaidi wa kidijitali na kutumia ubunifu ili kukuza uongozi wao na ujuzi wa biashara. Kwa vitendo, hadi sasa, vyama viwili vipya vya uzalishaji wa kakao inayolimwa kwa mbolea ya kiasili vimeanzishwa chini ya mradi huu.

Tangu mpango huu ulipoanza, mradi umefaidisha moja kwa moja watu 1,743 na takriban ekari 317 za misitu zimeboreshwa au kudumishwa katika mikoa ya Agnéby-Tiassa, La Mé na Sud-Comoé, pamoja na karibu ekari 1,400 za mashamba ya kawaida ya kakao kubadilishwa kuwa kilimo cha misitu au mifumo ya kilimo-ikolojia.

Ufyekaji wa misitu ya kitropiki kwa mashamba ya kakao yenye jua zima kumekuwa kichocheo kikubwa cha ukataji miti. Mradi wa FAO-GCF umeona karibu hekta 1,400 za mashamba ya kakao ya kawaida yakibadilishwa kuwa kilimo mseto au mifumo ya ikolojia ya kilimo.
©FAO/Zana Ouattara
Ufyekaji wa misitu ya kitropiki kwa mashamba ya kakao yenye jua zima kumekuwa kichocheo kikubwa cha ukataji miti. Mradi wa FAO-GCF umeona karibu hekta 1,400 za mashamba ya kakao ya kawaida yakibadilishwa kuwa kilimo mseto au mifumo ya ikolojia ya kilimo.

Kupunguza kiwango cha hewa ukaa katika uzalishaji wa kakao ni muhimu kwa kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Wakati huo huo, kuboresha ufuatiliaji kupitia aina mbalimbali za uthibitisho ni muhimu katika kuboresha uendelevu wa mnyororo wa ugavi wa kakao na kukuza kakao ya haki.

FAO inasema ikichochewa na mahitaji ya usafirishaji nje ili kukidhi watumiaji wa chokoleti duniani, ukataji wa misitu minene ya kitropiki kwa ajili ya mashamba ya kakao kwenye  jua kali umekuwa kichocheo kikubwa cha ukataji miti.

Lakini sasa, Muungano wa Ulaya EU, umeweka kanuni mpya za kukata miti (EUDR) ambazo zitakuwa na nguvu kufikia mwisho wa mwaka. Zinalenga kuhakikisha kuwa bidhaa zinazotumiwa na raia wa EU hazichangii katika ukataji miti au uharibifu wa misitu duniani kote.

Kwa kuwa nusu ya mauzo ya kakao ya nchi hiyo huenda EU, mpango wa PROMIRE's una dharura zaidi ya kufanya kazi ya ubunifu na wazalishaji kama Monique ili kubadilisha mlolongo wa kuongeza thamani ya kakao, kuimarisha ufuatiliaji, kulinda misitu na kupunguza mabadiliko ya tabianchi