Mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza mwezi huu wa Septemba hadi wiki ya pili ya mwezi Septemba mwakani. Katika ukurasa huu hata hivyo tutakuwa tunakuletea habari motomoto kutoka mjadala wa wazi na vikao vya ngazi ya juu vya mkutano huo ambavyo vinafanyika kuanzia tarehe 25 septemba 2018 hadi Oktoba mosi 2018. Pamoja na hotuba za viongozi ni vikao vya ngazi ya juu kuhusu Kifua Kikuu, Ulinzi wa Amani, tukio maalum la kumuenzi hayati Nelson Mandela na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs.
MKUTANO WA 73 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Marekani inaendeshwa na wamarekani: Trump
Marekani inaendeshwa na Wamarekani na ukiheshimu uhuru wetu hatutokuingilia wala kukwambia la kufanya. Kauli hiyo imetolewa leo na Rais wa Marekani Donald Trump alipouhutibia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
Vijana wa sasa si wa kusubiri kufunguliwa milango- Rais Ramaphosa
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amehutubia mjadala mkuu wa Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa ikiwa ni mara ya kwanza tangu achaguliwe kushika wadhifa huo akisema kuwa vijana wa sasa si wale wa kusubiri kufunguliwa milango.
Je Afrika ni tishio kubwa? Ahoji Rais Mutharika
Malawi imesema inaunga mkono msimamo wa Afrika wa kutaka kuwepo kwa wajumbe wawili wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na 5 wasio na kura turufu.
Naona mustakabali mkubwa ambao unaongozwa na vijana-Restless Development
Umoja wa Mataifa Jumatatu hii umezindua mkakati wake mpya kuhusu vijana ukilenga kuimarisha mchango wa takribani vijana bilioni 2 duniani kwa lengo la kukuza amani, uadilifu pamoja na kuwa na dunia endelevu. Mkakati huo umepatiwa jina, “Vijana 2030:Mkakati wa Umoja wa Mataifa kwa vijana,” umeshuhudiwa na viongozi wa nchi na wakuu wa serikali, lakini pia vijana ambapo mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo la kihistoria kutoka shirika la kiraia la Restless Development amezungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii punde tu baada ya tukio hilo na anaanza kwa kujitambulisha.
Sensa ya kilimo ni ndoto kwa baadhi ya mataifa maskini, na huu ni mkwamo - FAO
Ukosefu wa takwimu kuhusu kilimo unazuia juhudi za kutekeleza ajenda ya Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu.
Tunapinga umataifa na tunakumbatia uzalendo: Trump
Marekani inaendeshwa na Wamarekani na ukiheshimu uhuru wetu hatutokuingilia wala kukwambia la kufanya. Kauli hiyo imetolewa leo na Rais wa Marekani Donald Trump alipouhutibia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
Nahisi nawajibika na kifo cha kila mlinda amani- Guterres
Umoja wa Mataifa na nchi zinazochangia kwenye operesheni za ulinzi wa amani wa chombo hicho leo wamekuwa na kikao cha ngazi ya juu kuangazia jinsi ya kuimarisha operesheni hizo.
Hebu na tuyaangazie mambo chanya barani Afrika- Kagame
Rais Paul Kagame wa Rwanda amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kutaka kile alichokiita kuwa maendeleo chanya barani Afrika kisipuuzwe licha ya changamoto zinazokumba bara hilo.
Ushirikiano wa kimataifa ndio suluhu ya changamoto zinazotukabili:Espinosa
Misingi mikuu mitatu ambayo ni uongozi bora, kushirikiana majukumu na kuchukua hatua za pamoja ni muhimu kwa mustakhbali wa dunia amesema Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Maria Espinosa.
Si hiyari, ni lazima kulikabili jinamizi la mabadiliko ya tabia nchi:Guterres
Mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 73 umefunguliwa rasmi hii leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Wawakilishi kutoka nchi 193 wanachama, mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia na wadau wengine wa maendeleo wakikutana kwa lengo la kuhakikisha ajenda ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa inatimia ifikapo 2030.
Pagination
- 1
- 2