Skip to main content

Tunapinga umataifa na tunakumbatia uzalendo: Trump

Rais wa Marekani Donald Trump akihutubia mjadala wa wazi wa baraza Kuu la Umoja wa Mataifa 25 Septemba, 2018
Picha UN/Cia Pak
Rais wa Marekani Donald Trump akihutubia mjadala wa wazi wa baraza Kuu la Umoja wa Mataifa 25 Septemba, 2018

Tunapinga umataifa na tunakumbatia uzalendo: Trump

Masuala ya UM

Marekani inaendeshwa na Wamarekani na ukiheshimu uhuru wetu hatutokuingilia wala kukwambia la kufanya. Kauli hiyo imetolewa leo na Rais wa Marekani Donald Trump alipouhutibia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Trump ambaye hotuba yake imegisia masuala mbalimbali kuanzia usalama wa kimataifa hadi masuala ya wakimbizi na wahamiaji , ugaidi na masuala ya nyuklia amewaeleza wakuu wa nchi na serikali kwenye mjadala huo kwamba nchi yake inatoa kipaumbele kwa maslahi yake na watu wake na si vinginevyo

“Marekani inaongozwa na Wamarekani , tunapinga fikra zozote za ukimataifa na kukumbatia sera za uzalendo. Duniani kote mataifa ambayo yanawajibika ni lazima yajitetee dhidi ya vitisho vya uhuru wao , sio tu kutoka kwa utawala wa kimataifa lakini pia kutoka kwa aina mpya za ukandamizwaji na kutawaliwa.”

Wakati huohuo akarejelea kusisitiza dhamira ya Marekani ya kuhakikisha Umoja wa Mataifa unakuwa dhabiti na unaowajibika kwani anaamini Umoja huo una kila fursa ya kuwa hivyo.

Taswira ya Baraza Kuu pindi viongozi wa dunia wanapohutubia mjadala mkuu
UN/ Amanda Voisard
Taswira ya Baraza Kuu pindi viongozi wa dunia wanapohutubia mjadala mkuu

 

Kuhusu masuala ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa hakusita kuweka wazi msimamo wake wa kutotaka kuzogomwa

“Tulijiengua kwenye Baraza la Haki za Binadamu na hatutorejea hadi mabadiliko halisi yatakaanza kutekelelezwa na sababu hizohizo Marekani haitotoa msaada wowote wala kuitambua mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Kwa mujibu wa Marekani ICC haina uhalali na haina mamlaka.”

Kwa upande wa vita vya nyuklia ameipongeza Korea Kusini kwa kufanikisha jitihada za Marekani na Jamhuri ya watu wa Korea DPRK kupunguza mvutano uliodumu kwa muda mrefu kwa kusema “tumepuga hatua kubwa na sote tumeafikiana ni muhimu kuachana na sialaha za nyuklia kwenye rasi ya Korea.”

Na suala la uhamiaji ameitaka dunia kuheshimu maamuzi na matakwa ya taifa lake

 ‘Na hii ni moja ya sababu Marekani haitoshiriki kwenye mkataba mpya wa kimataifa wa uhamiaji . Uhamiaji haupaswi kusimamiwa na chombo cha kimataifa ambacho hakiwajibiki kwa wananchi wetu. Suluhu pekee ya kudumu ya mgogoro wa uhamiaji ni kuwasaidia watu kujenga matumaini ya mustakabali wao kwenye nchi zao na kuzifanya nchi hizo kuwa bora tena.”

Na kwa washirika wasiolipa fadhila amewapa onyo kwamba “tunazitetea nchi hizo bure kabisa bila faida yoyote, wengine wanatupandishia bei za mafuta na bidhaa , ni muhimu wapunguze gharama hizo kwani hatutokubaliana na hali hiyo.”

Ameongeza kuwa kamwe Marekani haitoomba radhi kwa kulinda maslahi ya watu wake.