Sensa ya kilimo ni ndoto kwa baadhi ya mataifa maskini, na huu ni mkwamo - FAO

Sekta ya kilimo inaajiri watu wengi lakini takwimu zinakwamisha sekta hiyo.
FAO/Olivier Asselin
Sekta ya kilimo inaajiri watu wengi lakini takwimu zinakwamisha sekta hiyo.

Sensa ya kilimo ni ndoto kwa baadhi ya mataifa maskini, na huu ni mkwamo - FAO

Ukuaji wa Kiuchumi

Ukosefu wa takwimu kuhusu kilimo unazuia juhudi za kutekeleza  ajenda ya Umoja wa Mataifa  kuhusu maendeleo endelevu.

 

Ameyasema hayo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa-FAO, Jose Graziano da Silva, leo mjini New York Marekani, katika mkutano wa kutafuta pesa kufadhili mipango ya shirika hilo. Lengo ni kuchangisha dola 500,000.

Katika mkutano huo FAO imeungana na washirika wengine, kama vile Benki ya Dunia, na taasisi ya Melinda  na Bill Gates ili kuunganisha juhudi za kukusanya data kwa pamoja kwa lengo la  kusaidia  maendeleo  ya lengo namba mbili la maendeleo endelevu, la kutokomeza njaa.

Graziano da Silva ameonya kuwa, changamoto katika upatikanaji wa takwimu bora, “husababisha mataifa yenye kipato cha chini, yashindwe kutoa mikakati sawa ya kimaendeleo na kuweza kuweka maamuzi sawa kuhusu sera au kuweza kufuatilia  maendeleo katika sekta ya kilimo.”

Taarifa zaidi kutoka FAO zinaeleza kuwa  kila mwaka  dola karibu bilioni 240 huwekezwa katika sekta ya kilimo kwenye mataifa ya kipato cha chini na wastani, lakini uamuzi wa uwekezaji muhimu unachukuliwa  bila kujali sekta hiyo.

Pia ukusanyaji wa takwimu za kilimo, anasema, bado ni  wa kiwango cha chini katika mataifa mengi ambapo mataifa mengi maskini takriban 75 hayajafanya sensa zao za kilimo za kila mwaka  kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita.

Kutokana na hali hiyo Mkurugenzi Mkuu wa FAO amesema, “tunahitaji kuchukua hatau zaidi ya hapo ili kuweza kuziba pengo kati ya mataifa yenye kipato cha chini na yale ya kipato cha kadri.

 

 

Tags: FAO, Jose Graziano da Silva, Bill Gates.