Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taka zaepusha matumizi ya dizeli Uganda

Taka zaepusha matumizi ya dizeli Uganda

Pakua

Matumizi ya nishati mbadala na salama ni jambo ambalo linapigiwa chepuo na Umoja wa Mataifa ambapo lengo namba 7 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linasisitiza nishati rahisi na salama. Hatua hii inazingatia kwamba idadi ya watu wanaohitaji nishati ya umeme inaongezeka kila siku na hivyo kutoa changamoto ya kusaka vyanzo mbadala vya nishati kwani umeme pekee uliozoeleka ni wa vyanzo vya maji, na ukame unatishia uwepo wa mabwawa ya maji. Ni kwa kuzingatia hilo huko Uganda, wanatumia mabaki ya taka au biomasi ili kuzalisha nishati. Je nini kinafanyika? John Kibego kutoka Uganda anaangazia ufanikishaji wa lengo hilo sambamba na lile la 13 la hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
3'16"
Photo Credit
UN Photo/Sophia Paris