Saidieni kupambana na uharibifu wa mazingira: Guterres
Tuna haki ya kuishi sehemu salama, tunategemea kula chakula bora, maji safi na kuvuta hewa safi lakini bado tunaendelea kuharibu mazingira.
Huo ni ujumbe wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika mkutano mkuu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa unaofanyika Nairobi, Kenya.
Guterres amesema tayari kuna mbinu na maazimio madhubuti za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoweza kuigwa kuinusuru dunia isiendelee kuathirika.
Amewaasa wajumbe wa mkutano huo kuwa dunia inawategemea katika kutoa matamko yatakayo zifanya nchi wanachana kulinda mazingira.