Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Mtambo wa makaa ya mawe Tuzla, Bosnia
UNEP

Bila kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa kwa asilimia 7.6 lengo la nyuzi joto 1.5 halitafikiwa-Ripoti ya UNEP

Katika kuelekea mwaka ambao mataifa yataimarisha ahadi zao za ulindaji wa hali ya hewa zilizoafikiwa mjini Paris, ripoti mpya iliyotolewa hii leo mjini Geneva Uswisi na shirika la Mpango wa mazingira wa Umoja wa Mataifa, UNEP, imeonya kuwa, ulimwengu utashindwa kufikia lengo la nyuzi joto 1.5 la mkataba wa Paris ikiwa dunia haitapunguza hewa chafuzi kwa asilimia 7.6 kila mwaka kati ya mwaka 2020 na 2030.

USGS/NASA

Asante Benki ya Dunia sasa tunaweza kufungua macho yetu- Wakazi Ningxia, China

Suala la kuenea kwa jangwa ni tatizo ambalo linakumba maeneo mbalimbali duniani kutokana na sababu kadhaa ikiwemo ukataji miti hovyo, ufugaji wa kuhamahama na mabadiliko ya tabianchi. Jamii ndio huathirika zaidi kama ilivyo katika eneo moja huko nchini China ambako jangwa lilienea katika enoe kubwa na hata kusababisha wakazi kupoteza njia za kujipatia kipato, na baya zaidi upepo wa jangwani ukiambatana na vumbi ulikuwa  hatari zaidi kwa macho yao. Hata hivyo Benki ya Dunia ilichukua hatua na kuleta kicheko kwa wakazi wa eneo hilo kama anavyosimulia Grace Kaneiya.

Sauti
3'48"

18 NOVEMBA 2019

Miongoni mwa Habari anazokuletea Flora Nducha katika Jarida la Habari hii leo

-Miaka 30 ya mkataba wa Haki za mtoto duniani CRC, kuna mafanikio kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF  lakini pia changamoto zinaendelea kwa watoto masikini

-Muungano wa Afrika AU na shirika la afya duniani WHO waanzisha ubia mpya ili kushirilkiana katika kutimiza malengo ya afya 

-Wakimbizi Sudan Kusini wasema wameambiwa amani imerejea Yambio sasa wanaanza kurejea nyumbani je nini wanakikuta huko?

Sauti
11'18"