Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
Ripoti mpya yaonesha kuna ongezeko la ishara na madhara ya mabadiliko ya tabianchi katika anga, ardhi na baharini
Ishara za mabadiliko ya tabianchi kama vile ongezeko la joto la ardhini na baharini, kuongezeka kwa kina cha bahari na kuyeyuka kwa barafu, vimeangaziwa katika ripoti mpya ya Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO na wadau wake iliyotolewa hii leo Machi 10 mjini New York Marekani na Geneva Uswisi.
Ripoti hiyo imeeleza madhara ya matukio ya hali ya hewa na tabianchi kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, afya ya binadamu, uhamiaji na ukosefu wa makazi, uhakika wa chakula, ardhi na maisha ya viumbe vya majini.
Tarajieni joto kali katika miezi ijayo:WMO
Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO leo limetoa tahadhari kwamba joto la kupita viwango vya wastani litarajiwe kwenye sehemu nyingi duniani katika miezi michache ijayo hata kama hakutokuwepo na matukio ya El Niño.
Mradi wa ProPESCA wabadili maisha ya wavuvi Msumbiji:IFAD
Mradi unaoendesha na mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD ujulikanao kama ProPESCA umebadili maisha ya wavuvi wengi wanaoshi katika mwambao wa Msumbiji waliohofia uvuvi wa kupindukia na mabadiliko ya tabianchi.
Ni wakati wa dunia kufuata nyayo za Pakistan kuhusu wakimbizi:Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres amesema anaamini kwa dhati kuwa huu ni wakati wa dunia kutafakari na kuiangalia Pakistan katika wigo mpana zaidi na kufuata nyayo zake hasa katika suala la kukirimu wakimbizi.
Ukarimu wa Pakistan kwa wakimbizi haukujali gharama wala usalama:Guterres
Kwa miaka 40 Pakistan imekuwa ikihifadhi mamilioni ya wakimbizi wa Afghanistan na ukarimu wao haukujali gharama za mzigo huo za kiuchumi au hatari za kiusalama amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
IFAD yatoa ombi la msaada kwa ajili ya kuimarisha maisha ya watu vijijini
Mfuko wa maendeleo ya kilimo duniani, IFAD unatoa wito kwa nchi wanachama kusaidi kuimarisha juhudi zake maradufu kwa ajili ya maisha ya watu wa jamii zilizotengwa kufikia mwaka 2030.
Antarctic yavunja rekodi ya kiwango kikubwa cha joto nyuzi joto 18.3C
Hofu mpya ya athari za mabadiliko ya tabianchi katika sayari dunia imechochewa na thibitisho la shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kwamba Antarctic imeshuhudia viwango vya rekodi mpya ya joto Kali ambalo limepindukia zaidi ya nyuzi 18C .
Kuanzia Libya, Yemen, Syria zahma imeighubika dunia: Guterres
Ni lazima tuvinje mzunguko wa machafuko na zahma zinazoighubika dunia hivi sasa , “leo hii upepo mbaya imevamia dunia” amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo akizungumza na waandishi wa Habari mjini New York Marekani.
UN yasema mabadiliko ya tabianchi na machafuko vyatumbukiza mamilioni kwenye njaa Sahel
Taarifa ya pamoja iliyotolewa leo na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa imeonya kwamba idadi ya watu wanaokabiliwa na upungufu wa chakula na fursa muhimu za Maisha Katikati mwa sahel imeongezeka sana katika mwaka mmoja uliopita kutokana na changamoto za usalama na mabadiliko ya tabianchi
Mabadiliko ya tabianchi na machafuko vyatumbukiza mamilioni kwenye njaa Sahel:UN
Taarifa ya pamoja iliyotolewa leo na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa imeonya kwamba idadi ya watu wanaokabiliwa na upungufu wa chakula na fursa muhimu za Maisha Katikati mwa sahel imeongezeka sana katika mwaka mmoja uliopita kutokana na changamoto za usalama na mabadiliko ya tabianchi.