Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Joto kali latarajiwa msimu wa kiangazi mwaka huu:WMO

Joto kali linatarajiwa katika msimu wa kiangazi mwaka huu 2018 kuanzia  Juni, Julai na Agosti, huku theluji katika maeneo ya Arctic ikiwa chini ya kiwango cha kawaida.

Mabadiliko ya tabianchi yaleta zahma kwa mamilioni 2017:UN

Mwaka wa 2017 umeelezwa kama ulioshudia matukio yaliyofurutu ada ya hali ya hewa na hivyo kuwafanya mamilioni ya watu duniani kuteseka. Hivyo Umoja wa Mataifa unasema si hadhithi tena bali athari za mabadiliko ya tabia nchi zimeanza kushudiwa hususan katika jamii zilizo hatarini zaidi.

Taka zaepusha matumizi ya dizeli Uganda

Matumizi ya nishati mbadala na salama ni jambo ambalo linapigiwa chepuo na Umoja wa Mataifa ambapo lengo namba 7 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linasisitiza nishati rahisi na salama. Hatua hii inazingatia kwamba idadi ya watu wanaohitaji nishati ya umeme inaongezeka kila siku na hivyo kutoa changamoto ya kusaka vyanzo mbadala vya nishati kwani umeme pekee uliozoeleka ni wa vyanzo vya maji, na ukame unatishia uwepo wa mabwawa ya maji. 

Sauti -
3'16"

Kilimo cha maharage ni matumaini ya wakulima Uganda

Kilimo cha maharage ni matumaini ya wakulima Uganda

Mataifa mengi ya kiafrika yanakabiliwa na tatizo la uhaba wa chakula moja ya sababu kubwa ikiwa ni athari ya mabadiliko ya tabia nchi.

Sasa wataalamu na watafiti wa nchini hizo wameanza kuchukua hatua ikiwemo ukulima wa mazo yanayohimili mabadiliko hayo kama maharagge.

Sauti -

Mwaka mmoja wa mkataba wa Paris, mafanikio ni dhahiri

Mwaka mmoja wa mkataba wa Paris, mafanikio ni dhahiri

Mkutano wenye lengo la kuchagiza utekelezaji wa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi utafanyika kesho mjini Paris, Ufaransa, ukienda sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutiwa saini kwa nyaraka hiyo.

Sauti -

Uhakika wa chakula na lishe ni changamoto kubwa Asia na Ulaya:FAO

Uhakika wa chakula na lishe ni changamoto kubwa Asia na Ulaya:FAO

Baadhi ya nchi za Ulaya na Asia ya Kati ni miongoni mwa nchi ambazo zimeathirika zaidi na  mabadiliko ya tabianchi, hali ambayo imesababisha uharibifu wa mazao, misitu na pia kuathiri sekta ya ufugaji na uvuvi.

Sauti -