Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

14 JANUARI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Grace Kaneiya anakuletea 

-Dola milioni 477 zahitajika ili kunusuru maisha ya takriban watu laki tisa nchini Sudan kwa mahitaji ya kibinadamu kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR lililozindua ombi hilo leo mjini Khartoum 

-Ofisi ya miradi ya Umoja wa Mataifa, UNOPS kwa kushirikiana na Benki ya dunia pamoja na wadau wenyeji, wanafanya juhudi za kuboresha huduma mijini pamoja na nishati ya umeme kwa mamilioni ya watu wa Yemen.

Sauti
10'41"
UN News/Assumpta Massoi

Je wajua kuwa ukubwa wa ziwa Tanganyika unazidi kupungua?

Nchini Tanzania, Ziwa Tanganyika lililopo mkoani Kigoma lasifika kwa kuwa la pili kwa kuwa na kina kikubwa zaidi duniani. Hata hivyo, kina na ukubwa wa ziwa vinapungua kutokana na mabadiliko ya tabianchi na shughuli za binadamu. Miongoni mwa mashuhuda wa hali hiyo ni Bwana  Kassim Govola Mbingo ambaye ni mhifadhi mkuu katika makumbusho ya Dkt. David Livingstone mjini Ujiji mkoani Kigoma. Katika mahojiano yake na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya  Umoja wa Mataifa anafafanua

Sauti
3'55"

13 JANUARI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Miaka 10 baada ya tetemeko baya la ardhi nchini Haiti athari zake zinaendelea kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM

-Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeutenga mwaka 2020 kuwa ni wa afya ya mimea kwa kutambua mchango na thamani ya mimea hiyo kwa maisha ya watu na syari dunia

-Maelfu ya Wavenezuela wakiwemo watoto wanaendelea kufungasha virago na kukimbilia nchi jirani ikiwemo Brazil limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF

Sauti
11'50"

09 JANUARI 2020

Katika Jarida letu la Habari hii leo Arnold Kayanda anakuletea 

-UNHCR yatoa changamoto kwa Muungano wa Ulaya kuufanya mwaka 2020 kuwa wa ulinzi kwa wakimbizi na wahamiaji

-Kuanza tena kwa doria inayojumuisha mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSCA ni neema na amani kwa raia 

-Nchini Burkina Fasso mradi wa pamoja wa shirika la chakula na kilimo FAO, Muungano wa afrika Au na serikali ya nchi hiyo kupambana na hali ya jangwa umeleta tija kwa wananchi

-Makala yetu hii leo inatupeleka Uganfa kumulika ugonjwa wa ukimwi , wakimbizi na sekta ya mafuta

Sauti
11'45"