Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyenzo mpya ya FAO kusaidia mazao aina mabalimbali kushamiri

Chakula cha asili kama quinoa kimekuwepo kwa karne nyingi , lakini limetelekezwa kwa sababu mazao mengine yanayozalishwa kwa wingi na yenye soko yamechukua nafasi katika mfumo wa kilimo
FAO/MINAG/Heinz Plenge
Chakula cha asili kama quinoa kimekuwepo kwa karne nyingi , lakini limetelekezwa kwa sababu mazao mengine yanayozalishwa kwa wingi na yenye soko yamechukua nafasi katika mfumo wa kilimo

Nyenzo mpya ya FAO kusaidia mazao aina mabalimbali kushamiri

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Nyenzo mpya ya shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, itawajengea mnepo wakulima na kulinda mazao kwa kwa kusaidia katika uendelezaji wa kilimo cha mazao mbalimbali na pia kuwasaidia wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuenzi mbinu za kiasili na mifumo ya kilimo.

Nyenzo hiyo ya FAO ni muongozo mpya uliochapishwa leo mjini Roma Italia kwa lengo la kuhakikisha mazao ya aina mbalimbali yanalimwa na kuwajengea mnepo wakulima kupanda mazao ya asili yanayotoweka.

Muongozo huo umepewa jina “Muongozo wa hiyari kwa kuhifadhi na matumizi endelevu ya wakulima kwa mazao mbalimbali” ni msaada mkubwa kwa mipango ya nchi katika mataifa yanayoendelea ya kulinda rasilimali hizo muhimu za mazao.

Kwa mujibu wa FAO mazao hayo ni yale yanayoweza kuvumilia mabadiliko ya kimazingira na yana uhusiano na ujuzi wa asili kuhusu hulka ya wakulima, uchaguzi wa mbegu na udhibiti wa mashamba.

Dawa za kuulia wadudu wanaoshambulia mazao zinapaswa kuwekewa maelezo ya kutosha ili zisiwe na madhara kwa watumiaji
UNDP Uganda/Luke McPake
Dawa za kuulia wadudu wanaoshambulia mazao zinapaswa kuwekewa maelezo ya kutosha ili zisiwe na madhara kwa watumiaji

Hali tofauti ya wakulima kudhiditi mazao mbalimbali inajumuisha kutambua mifumo mbalimbali ya kilimo , mazingira, machaguo yanayofanywa na wakulima, utunzaji wa mbegu na kubadili mifumo, na kutunza upatikanaji wa mbegu za mazao hayo ambayo mengine ni ya asili.

Hilo linatoa mchango mkubwa kwa chakula na uhakika wa lishe, kusaidia maisha vijijini, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na hata kusaidia watu kuishi.

Mazao hayo yanatambulika kwa majina ya asili na kuhusishwa na matumizi ya kiasili , ujuzi, hulka na kuwasherehekea watu walioanzisha  na kuendelea kuyakuza mazao hayo.

Idadi kubwa ya mazao ya asili hupotea

Hata hivyo shirika la Fao linasema idadi kubwa ya mazao hayo ya asili hupotea au kutelekezwa na kusababisha hatari kubwa katika mustakbali endelevu wa mifumo ya chakula.

Tijani Bukar mkurugenzi msaidizi wa FAO kitengo cha kilimo na ulinzi kwa walaji amesema “Mifumo ya chakula leo hii inaambatana na tabia za kuwa na mazao yanayofanana na aina tofauti za mashamba. Ili kuwa endelevu wakulima ni lazima walime mazao ambayo yana asili tofauti ambayo yanaendana na mazingira yao, mfumo wa uzalishaji na yanayopendwa na watumiaji.”

Mazao ya DPRK kama vile mpunga, mahindi, soybean na viazi yameharibiwa sana kufuatia ukame uliokithiri.
FAO/ Cristina Coslet
Mazao ya DPRK kama vile mpunga, mahindi, soybean na viazi yameharibiwa sana kufuatia ukame uliokithiri.

Tijani ameongeza kuwa aina tofauti za mazao ya kiasili ni shina la kujaribu kulima mazao mengine tofauti. Na hukla hiyo sio tu kwamba inasaidia matumizi ya ya chakula cha asili lakini pia inaongeza mnepo na uwezo wa kukabili wadudu wa mimea, magonjwa na mabadiliko ya tabianchi.

Mtazamo Madhubuti

FAO inasema muongozo huu mpya wa hiyari ulizinduliwa  leo kandoni mwa kikao cha 8 cha bodi ya udhibiti ya mkataba wa kimataifa kuhusu rasilimali  asilia za mimea kwa ajili ya chakula na kilimo.

Na umetoa mapendekezo kadhaa kuanzia kubaini na kuweka kumbukumbu ya aina za rasilimali za mimea zilizopo kwa ajili ya kilimo , ramani ya uwezekano wa matumizi yake  , uchagizaji wa kudumu kwake na kuwapa wakulima na jamii taarifa na msaada unaohusiana na utunzaji wao na matumizi endelevu kwa kuzingatia utaalam na vipaumbele vya taifa.

Muongozo huu mpya ni wa kwanza wa aina yake kuelezea mtazamo wa aina hii.