COP26 ikifungua pazia WMO yasema miaka 7 iliyopita imevunja rekodi ya joto duniani
COP26 ikifungua pazia WMO yasema miaka 7 iliyopita imevunja rekodi ya joto duniani
Miaka saba iliyopita inaelekea kuwa ya joto zaidi kuwahi kurekodiwa sanjari na kupanda kwa kina cha bahari ni katika viwango vya kuvunja rekodi, kulingana na ripoti ya muda ya shirika la hali ya hewa duniani (WMO) ya hali ya hewa duniani kwa mwaka 2021, iliyotolewa Jleo umapili, wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26, ukifunguliwa Glasgow, Uingereza.
Kwa mujibu wa WMO, viwango gesi chafuziya viwandani angani ambavyo havijawahi kushuhudiwa na mkusanyiko wa ongezeko la hali ya joto vimeifanya sayari hii kuwa katika eneo lisilojulikana, na kusababisha madhara makubwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Ripoti ya muda ya WMO, ambayo imetokana na takwimu za miezi tisa ya kwanza ya mwaka, inabainisha kuwa kutokana na kupoa kwa muda kunakohusishwa na kipindi cha La Niña kilichoshuhudiwa mwanzoni mwa mwaka, 2021 hakitaendelea.
Pengine utapata kwamba uko katika nafasi ya tano kwenye orodha ya miaka saba iliyokuwa na joto zaidi katika rekodi.
Hata hivyo, mwelekeo wa muda mrefu wa kuongezeka kwa joto hautarudi nyuma wala kudhoofishwa.
Kupanda kwa kina cha bahari duniani kote, ambacho kimekuwa kikiongezeka tangu 2013, kulifikia rekodi mpya mwaka 2021, sambamba na mchakato wa kuongeza kwa kiwango cha joto natindikali ya bahari.
Ripoti hiyo imetolewa kutokana na michango kutoka kwa mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa, huduma za kitaifa za hali ya hewa na maji na wataalam wa kisayansi. Inaangazia athari za ongezeko la joto duniani katika uhakika wa chakula na kutawanywa kwa idadi kubwa ya watu, ambayo huharibu mifumo muhimu ya ikolojia na kuathiri kufikiwa kwa malengo ya maendeleo endelevu.
"Ripoti hiyo ya muda ya WMO kuhusu hali ya hewa duniani kwa mwaka 2021, kutokna na takwimu za hivi karibuni za kisayansi, inaonyesha kwamba sayari yetu inabadilika mbele ya macho yetu. Kuanzia kupanda kwa kina cha bahari hadi katika vilele vya milima, viko chini ya athari isiyoweza kuepukika ya kuyeyuka kwa barafu na hali mbaya ya hewa, kote duniani mifumo ya ikolojia na idadi ya watu wa sayari hii viko katika shinikizo kubwa. COP26 lazima iwe alama ya mageuzi madhubuti kwa binadamu na sayari hii ", amesisitiza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres.
Suluhisho liko mikononi mwako
"Wanasayansi wana uhakika wa hitimisho lao. Viongozi wanatakiwa kujiamini vivyo hivyo katika maamuzi yao. Mlango uko wazi: suluhisho zinapatikana. COP26 lazima itie alama kwenye hatua madhubuti ya mageuzi. Hebu tuwe na tamaa. Tuoneshe mshikamano. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua ili kuhifadhi mustakabali wetu na kulinda ubinadamu, "ameongeza Guterres katika ujumbe wake wa video kuhusu ripoti hiyo.
Katibu Mkuu wa WMO Petteri Taalas amebainisha kuwa "kwa mara ya kwanza tangu takwimu hizo kurekodiwa, theluji ilinyesha kwenye sehemu ya juu kabisa ya barafu ya Greenland, ambapo haijawahi kunyesha".
Ameongeza kuwa "Nchini Canada, barafu inayeyuka haraka. Wimbi la joto lililokumba Canada na maeneo jirani ya Marekani lilipandisha hali ya joto hadi karibu nyuzi joto 50 ° C katika kijiji kimoja huko British Columbia. Katika Bonde la Kifo, California, hali ya joto ilifikia nyuzi joto 54.4 ° C wakati wa mojawapo ya mawimbi mengi ya joto ambayo yalipiga kusini-Magharibi mwa Marekani, huku maeneo mengi karibu na Mediterania yakishuhudia hali ya joto iliyovunja rekodi. Joto hili la kipekee mara nyingi liliambatana na moto mbaya wa nyika.”
Mkuu huyo wa WMO pia amebainisha kuwa nchini China, " Mvua kubwa ilinyesha kwa saa chache kwa kiwango ambacho kwa kawaida hunyesha katika miezi kadhaa na sehemu za Ulaya zimekumbwa na mafuriko makubwa.”
Majanga haya yaligharimu maisha ya makumi ya watu na kusababisha hasara ya kiuchumi inayofikia mabilioni ya euro.
Katika hali ya joto ya Amerika Kusini, “kwa mwaka wa pili mfululizo wa ukame ulipunguza mtiririko wa maji katika maeneo muhimu na kuathiri kilimo, usafiri na uzalishaji wa nishati, "amesema Bwana. Taalas.
Amekumbusha kuwa "hakuna kitu cha kipekee juu ya matukio yaliyokithiri. Ushahidi zaidi na zaidi wa kisayansi unathibitisha kwamba baadhi ya matukio haya ni ishara ya mabadiliko ya tabianchi," ameongeza.
Amesisitiza kuwa "Ikiwa viwango vya gesi chafu vitaendelea kuongezeka kwa kiwango cha sasa, ongezeko la joto litakuwa limevuka kwa kiasi kikubwa kikomo kilichoainishwa na malengo ya mkataba wa Paris cha nyuzi joto (1.5 hadi 2 ° C juu ya viwango vya kabla ya maendfeleo ya viwanda) ifikapo mwishoni mwa karne," alisema Bw. Taalas "COP26 inatupa fursa madhubuti ya kurudi kwenye njia sahihi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi".