COP26 – Tunachofahamu kwa sasa, na kwa nini ni muhimu: Muongozo wako wa habari kutoka Umoja wa Mataifa

COP26 – Tunachofahamu kwa sasa, na kwa nini ni muhimu: Muongozo wako wa habari kutoka Umoja wa Mataifa
Katika dunia iliyotikiswa na mliipuko na kuwa dirisha lililofuga fursa za kupambana na majanga ya tabianchi, mkutano muhimu wa Umoja wa Mataifa wa COP26 unang’oa nanga leo Jumapili katika mji wa Glasgow nchini Scotland madhara ya janga hilo yasingekuwa makubwa zaidi kama yalivyo sasa.
“Bila uamuzi, tunachezea fursa yetu ya mwisho ya kubadili hali iliyopo”, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres kabla ya kuanza kwa COP26. Je, ni jinsi gani inaweza kuwa fursa yetu ya mwisho?
Hili hapa jawabu la masuali ambayo tumegundua kuwa ndio hua yanaulizwa na unaweza kuwa nayo kuhusu kinachokuja.
Hebu tuanze na swali la msingi kwa mfano, COP26 ni nini?
Kwa urahisi kabisa , COP26 ni mkutano mkubwa na muhimu zaidi kuhusu mabadiliko ya tabianchi duniani.
Mwaka 1992, Umoja wa Mataifa uliandaa tukio kubwa mjini Rio de Janeiro lililotwa “Earth Summit” yani Kongamano la Sayari Dunia, ambapo mkataba wa mwongozo wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi (UNFCCC) ulipitishwa.
Katika mkataba huo, walikubaliana "kuweka juhudi za kupunguza gesi ya viwandani angani” kuzuai athari ya shughuli za binadamu kwa mfumo wa tabianchi. Na tunavyoendelea, mkataba huo umerishdhiwa na nchi 197.
Tangu mwaka 1994, ambapo mkataba huo ulianza kutekelezwa, kila mwaka Umoja wa Mataifa umekuwa ukizileta karibu nnhci zote duniani kuhudhuria mikutano kuhusu tabianchi au “COPs”, ikimaanisha ‘Mkutano wa Washirika’.
Mwaka huu ungekuwa mkutano wa 27th wa kila mwaka lakini kutokana na mlipuko wa COVID-19, ulihairishwa mwaka moja na hivyo mwaka huu umekuwa COP26.

Nini hufanyika kwneye COP26? Je, hatuna mikutano inayotosha kuhusu mabadiliko ya tabianchi tayari?
Mara kadhaa “kupanua wigo wa ajenda hiyo” kwenye mkataba wa UNFCCC kumejadiliwa kwenye mikutano ya COP ili kuweka viwano vya kisheria kuhusu utoaji wa gesi chafuzi ya viwandani kwa nchini husika na kubaini mikakati ya kutekeleza mkataba huo.
Haya ni pamoja na mkataba wa Kyoto wa mwaka 1997, ambao uliweka viwanngo vya mwisho vya nchi zilizoendelea kutoza gesi chafuzi vinavyotakiwa ifikapo 2012; na Mkataba wa Paris, uliopitishwa mwaka 2015 ambapo mataifa yote duniani yalikubaliana kuweka mikakati ya kudhibiti kiwango cha hali ya joto duniani kwa nyuzi joto 1.5°C juu ya viwango kabla ya mapinduzi ya viwanda na kuongeza uwekezaji katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa hiyo hapa ndipo COP26 inavutia wakati wa mkutano. Miongoni mwa mengine, wajumbe watakuwa na lengo la lukamilisha ‘Kitabu cha kanuni za mkataba wa Paris’, hasa kwa kanuni zinazohitakika kutekeleza mkataba huo.
Kwenye mkutano wa mwaka huu itawabidi kukubaliana kuhusu muda kwa mikutano ya kudurusu mkataba huo na kufuatilia ahadi zao kuhusu tabianchi.
Kimsingi, Mkataba wa Paris uliweka ukomo, na kudhibiti wa kiwango cha joto duniani hadi chini ya nyuzi joto mbili, (yani 1.5) lakini Glasgow, ni fursa ya mwisho kufanikisha miundombinu ya kutimiza ndoto hiyo.

Kwa hiyo hii inatukaribisha kwenye swali letu la msingi: Kwa nini fursa hii ni ya mwisho?
Kama dubu anavyojisogeza polepole kufanya mawindo yake hadi kifo, mabadiliko ya tabianchi yamegeuka kutoka kuwa kitu kinachofanya maisha magumu kwa kiasi kidogo na kuwa dharura ya ulimwengu inayotishia uhai, katika miongo miatatu iliopita.
Ingawa kumekuwepo ahadi mpya na zilizorekebishwa zikitolewa na nchi mbele ya COP26, dunia imesalia kwenye hatari ya ongezeko la joto duniani la angalau nyuzi joto 2.7°C katika karne hii ingawa Paris malengo yamefikia.
Sayansi iko bayana: ongezeko la hali ya joto kiasi hicho mwishoni mwa karne kunaweza kumaanisha miongoni mwa mengine, ongezeko la asilimia 62% la mioto ya nyika katika maeno ya Kaskazini ya sayari dunia katika majira ya joto, kupoteza makaazi ya theluthi tatu ya wanyama duniani, na kame za kati ya miezi 4 hadi 10.
Katibu Mkuu wwa Umoja wa Mataifa, António Guterres analitaja kuwa “janga la tabianchi”, kile kinachozikabili kwa kiwango kikubwa nchi zilizohatarini zaidi duniani kama vile maeneo ya kusini mwa Jnagwa la Sahara, nchi za kwenye visiwa vidogo vinavyotuama wakati wa ongezeko la viwango vya maji ya bahari.
Tayari mamiliioni ya watu wamefariki dunia au kupoteza makaazi kutokana na majanga yanayochochewa na mabadiliko ya tabianchi
Bwana Guterres, ameleza kuwa mamia ya wanasayansi kwneye Jukwa la kimataifa la mabadiliko ya tabianhci, kuhakikisha hali ya joto imesalai kuwa nyuzijoto 1.5°C ni mazingira pekee ya uhai wa binadamu”.
Saa inagonga, na ili kusalia na fursa ya kudhibiti ongezeko la joto, mataifa yanahitaji kushirikiana kubeba mzigo wa gesi chafuzi au gesi ya nyumba ya kijani katika miaka nane ijayo.
Hii ni kazi kubwa saaa ambayo tutaweza kufanya kwa ufanisi wakati viongozi wanaphudhuria COP26 ni kuleta mipango kabambne, itakayotekelezwa kwa muda kutokomeza matumizi ya makaa ya mawe na kubadili uchumi wao kufikia hadi kwa kile kitwacho kiwango cha kutotoa hewa yoyote chafuzi.

Je, nchi kama China na Marekani tayari zimeahidi kutozalisha kabisa hewa ukaa?
Ripoti ya hivi karibuni Zaidi ya Umoja wa Mataifa kuhusu pengo katika utoaji wa hewa chafuzi inaonesha kwmaba karibu nchi 49 pamoja na Muungano wa Ulaya zimeahidi kupunguza utoaji wa hewa chafuzi hadi sufuri kama lengo lao.
Hii ni karibu nusu ya utoaji wa gesi ya nyumba ya kijani kwa matumizi ya nyumbani duniani kote, zaidi ya nusu ya pato la ndani la duniani na robo tatui ya idadi ya watu duniani.
Malengo 11 yemewekwa katika sheria, yakiangazia asilimia 12 ya utoaji wa hewa chafuzi duniani.
Inaonekana kuwa muhimu sana ? Lakini kuna changamoto ambapo ahadi nyingi zinasubiri hadi 2030, zikizua wasiwasi kuhusu iwapo ahadi za kupunguza hadi sufuri zinaweza kufikiwa.
Pia baadhi ya ahadi hazina msingi na haziendani na ahadi zilizokabidhiwa rasmi zijulikanazo kama NDCs.
Hili kwa mara nyingine linaeleza kwa nini COP26 ni mkutano muhimu: “Muda wa diplomasia umepita.Ikiwa serikali hususani zile tajiri duniani za G20 hazitosimama na kuongoza juhudi hizi, tunaelekea kwneye majanga makubwa zaidi na kuumia kwa binadamu”, aonya Katubu Mkuu alipokuwa kwneye Mkutano wa Baraza la Umoja wa Matifa wiki hii.

COP26 inatazamiwa kupata mafanikio gani?
Majadiliano rasmi hufanyuka kwa wiki mbili. Wiki ya kwanza hutambulisha majadiliano ya kitaalamu ukishirikisha, mafisa wa serikali , yakifuatwa na mkutano wa ngazi ya juu wa mawaziri na Maraisi katika wiki inayofuata, ambapo maamuzi ya mwisho yatafanywa au la.
Kuna mambo manne muhimu ambayo yatajadiliwa katika mkutano huo kulingana na mwenyeji wake - Uingereza:
1. Kuhakikisha utokomezaji kabisa wa utoaji wa gesi chafuzi ifikapo nusu ya karne hii na kuhakikisha kiwango cha joto hakivuki nyuzi joto 1.5 kwa kila nchi
Ili kufanikisha hili nchi zinapaswa kutia bidi kuaacha kabisa matumizi ya “makaa ya mawe”, kuzuia ukataji wa misitu, kuharakisha hatua za kuelekea uchumi wa kijani zaidi. Mikakati ya kukuza soko la hewa ya ukaa pia itajadiliwa.
2. Weka mbinu zaidi kulinda jamii na makaazi asilia
Kwa sababu mabadiliko ya tabianchi yanashuhudiwa tayari kwneye nchi kadhaa, nchi hizo zinahitaji kulinda na kuchukua hatua za kurejesha upya maeneo yaliochafuliwa, na kujenga juhudi za ulinzi dhidi ya uhifahdi na miundombinu stahiki.
3. Kutayarisha ufadhili
Kwneye COP15, nchi tajiri duniani ziliahidi kuelekeza dola milioni 100 mwaka moja kwa nchi zinazoendelea ifikapo mwaka 2020 kuzisaidia kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kudhibiti ongezeko la joto.
Ahadi hiyo haikutimizwa, na COP26 utakuwa muhimu sana kuchangisha fedha, kwa msaad akutoka taaissi ya kifedha za kimataifa, na pia kuweka malengo mapya ya kufadhili juhudi za kudhibiti mabadiliko ya tabianhci ifikapo 2025.
4. Kushirikiana ili kupata mafanikio
Hii inamaanisha ushirikiano kai ya serikali, biahsara na asasi za kiraia, na vile vile kukamilisha kitabu cha kanuni cha Paris ili kuanza kutekeleza kikamilifu mkataba huo.
Juu ya hayo mazungmuzo rasmi, COP26 unatarajiwa kujenga mikatati mpya na ushirikiano ili kupata mafanikio katika hatua za kudhibiti mabadiliko ya tabianchi.

Vipi, lini na wapi?
Tukio kubwa kabisa na linafanyika kwneye ukumbi wa Scottish Event Campus, kuanzia 31 Oktoba hadi 12 Novemba, kukiwa na uwezekano mazungumzo kuendelea kwa siku moja au mbili zaidi. Kwa sasa kuna watu zaidi ya 30.000 waliosajiliwa kuhudhuria wakiwakilisha serikali, biashara, mashirika yasio ya kiserikali, na asasi za kiraia.
Nchi 197 zinazohusika na maktaba wa UNFCCC, hua zinafanya kazi kwenye vikundi kujadiliana huku nchi tajiri zaidi dunaini au G77 na China, kikundi cha Africa, nchi zilizomaskini zaidi, Umbrella Forum, Nchi za Visiwa vidogo vidogo zinazoendelea, na muungano huru wa nchi za Amerika ya Kusini na Caribbea.
Mazungumzo hayo pia yanashirikisha wangalizi, wasiokuwa na upande rasmi wa kujitegemea lakini wakichangia kwneye mazungmzo yanayosaidia kuleta uwazi.
Wangalizi hao ni pamoja na wakala wa Umoja wa Mataifa, mashirka ya kimataifa ya kiserikali, mashirika yasio ya kiserikali, mashirika ia kidini, na wanahabari.
Lakini kando na mazungmuzo rasmi, kutakuwepo mikutano mbalimbali na maelfu ya matukio, kwenye siku mbali mbali, kwenye mada kama vile fedha, nishati, vijana na uwezeshwaji wa umma, masuala ya asili, uhimili, jinisa, sayansi na ubunifu, usafiri, na miji.
Mkutano utafanika kwneye maeneo mawili Blue Zone (Scottish Events Campus), na Green Zone lililokaribu na kituo cha sayansi cha Glasgow.
Blue Zone ni eneo la tukio litakalosimamiwa na Umoja wa Matifa na ili kuingia kila atakayehudhuria ni lazima aidhinishwe na Viongozi wa UNFCCC.
Green Zone litasimamiwa na serikali ya Uingereza lakini likakuwa wazi kwa umma. Iitajumuisha matukio, maonesho, warsha na mijadala ya kukuza moyo wa mazungmuzo, uhamasishaji, kuelimisha, na kutoa ahadi kuhusu kukabiliana na mabadiliko ya tabianhci.
Kuna yoyote mshuhuri atakayehudhuria?
Marais wengi sana akiwemo waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na rais wa Marekan, Joe Biden wanatarajiwa kuhudhuria. Wengine ni pamoja na Sir David Attenborough, kundi la kutetea COP26, mwanaharakati Greta Thunberg.
Malkia alitangaza kuwa atasikitika kutokuwa hapo Jumatatu, kwamba asingeweza kusafiri kwenda kwenye eneo kubwa la tukio.
Balozi mpya wa Umoja wa Matafa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDG), Kundi maarufu la muziki toka Korea K-pop BLACKPINK nao watakuwa wakijiunga kwneye mkutano.
Kikundi cha wasichana cha Korea kilitoa video kuhusu tukio hilo kabla ya kuwasili, ikionesha jinsi walivyoguswa na mabadiliko ya tabianchhi huku wakitaka hatau zichukuliwe.

Je, kutakuwepo mikakati maalumu ya kudhibii COVID-19 kwenye mkutano mkubwa wa aina hiyo?
Huku COVID-19 ikisalia kuwa changamoto kubwa duniani kote, hatua za kuhsughulikia janga la haziwezi kusubiriwa kulingana na wenyeji wa COP26.
Mazungmuzo kupitia mitandaoni yatakubaliwa ili kuhakikisha ushiriki jumuishi wa watu kutoka nchini za kipato cha juu na zile za kipato cha chini na pia kuhakikisha usalama na uwazi.
Wanaohudhuria wanahimizwa wawe wamepata chanjo kamili na Uingereza ilifanya mpango wa kuwapatia dozi za chanjo washiriki wanaoishi katika nchi zisizoweza kupata chanjo hiyo.
Pia kutakuwepo mchakato wa kupima hali ya kila mtu ya COVID-19 ikiwemo kupima kila siku kwa kila anayeingia kwenye eneo la tukio la Blue Zone ili kuuhakikisha afya njema na maisha bora ya wote wanaohudhuria na jamii jirani.
Pia kuna mpango maalum wa COP-kuoona kwamba wanaosafiri kwelekea England na Scotland, kuhusu COVID-19 ambapo baadhi ya nchi zinawatia karantini lakini wataweza kusiadia kwa ufadhilii kutoka serikali ya Uingereza kwa ajili ya kuhakikisha wanasafiri kwa urahisi.
Je, Ninawezaje kufuatilia mijadala hiyo na matukio yote nikiwa nyumbani kwangu?