Skip to main content

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

20 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea maoni kuhusu matumizi ya lugha ya kiswahili kutokwa kwa viongozi wanaoshiriki UNGA78, na yaliyojiri hapa makao makuu katika mjadala kuhusu malengo ya maendeleo endelevu. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia hapa makao makuu, kulikoni?  

Sauti
14'56"
UN/ Stella Vuzo

Tuzungumze Kiswahili kwenye UNGA78 - Viongozi wa EAC

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki amesema ili kuongeza ushawishi na kukuza lugha ya Kiswahili duniani ni vyema viongozi wa jumuiya wakazungumza lugha hiyo wakiwa katika mikutano mikubwa duniani akitolea mfano mjadala Mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa au UNGA78.  

Sauti
3'36"
Habari za UN

Methali: "Ukubwa jalala"

Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Ukubwa ni jalala.”

Sauti
1'39"

11 JULAI 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo ninatupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kama ilivyo sehemu nyingi za Afrika Mashariki nako lugha ya kiswahili inatajwa kuwa chombo chenye nguvu sana kinachoingilia kati ujenzi wa amani na pia katika biashara hasa kwa wakaazi wa mji wa Goma katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Kiswahili ndio lugha ya kwanza nchini DRC yenye idadi kuwa ya wazungumzaji katika mikoa ya Mashariki na Magharibi mwa nchi ambako inatumiwa hata kwenye vyombo vya habari kama Redio na televisheni.

Sauti
10'50"
Habari za UN

MSEMO - Sikio halilali njaa

Na leo Katika jifunze Kiswahili tuko Baraza la Kiswahili la ZANZIBAR nchini Tanzania ambapo hii leo Dkt. Mwanahija Ally Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA anafafanua msemo “sikio halilali njaa.” 

 

Sauti
1'5"