Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

Habari za UN

MSEMO - Sikio halilali njaa

Na leo Katika jifunze Kiswahili tuko Baraza la Kiswahili la ZANZIBAR nchini Tanzania ambapo hii leo Dkt. Mwanahija Ally Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA anafafanua msemo “sikio halilali njaa.” 

 

Sauti
1'5"

02 FEBRUARI 2023

Hii leo katika Jarida tunakuletea Habari kwa Ufupi, Mada kwa Kina na Jifunze lugha ya Kiswahili.

Katika Habari kwa Ufupi Leah Mushi anamulika ziara ya Papa Francis nchini DR Congo na wito wake kwa vijana na viongozi wa dini kukataa rushwa. Halikadhalika anamulika maeneo oevu na umuhimu wake bila kusahau nchini Sudan Kusini ambako Umoja wa Mataifa unaendelea kutoa misaada kwa familia zilizokimbia kutoka katika eneo la Pibor.

Sauti
12'