Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutambulika kimataifa Kiswahili kitaongeza wageni watakaotaka kujifunza lugha hiyo:Ali Yusuf Mwarabu

Mwonekano wa maeneo ya forodhani visiwani Zanzibar.
UN News/Assumpta Massoi
Mwonekano wa maeneo ya forodhani visiwani Zanzibar.

Kutambulika kimataifa Kiswahili kitaongeza wageni watakaotaka kujifunza lugha hiyo:Ali Yusuf Mwarabu

Utamaduni na Elimu

Kuelekea Siku ya Lugha ya Kiswahili duniani itakayoadhimishwa Alhamisi ya wiki ijayo Julai 7 mmoja wa wakaazi wa Chukwani Zanzibar Ali Yusuf Mwarabu anasema hatua ya lugha hiyo kutambulika kimataifa kwanza ni Fahari kubwa kwa Wazanzibari lakini pia itakuwa ni fursa nzuri kwa wageni wanaoipenda kujifunza kwa urahisi kuanzia waliko na hata kufunga safari kwenda kisiwani humo.

 “Kwa wageni wengi wakija huwa wanapenda kusoma Kiswahili sasa kama kitakuwa kimeenea kila mahali itakuwa ni rahisi kwao pia wataanza kukisoma hukohuo kwao badala ya kutoka kwao kuja kukitafuta huku” 

Ali anasema ni muhimu sasa  lugha hiyo itumike mashuleni kama lugha rasmi na anafafanua kwa nini? “kwa sababu wanafunzi wengi wanafeli kwa kutooelewa lugha ya kigeni ya kiingereza inayofundishiwa mashuleni, labda ingekuwa inatumika hata mashuleni Kiswahili kitupu labda ufaulu pia ungeongezeka.Kwa hiyo kwa maoni yangu serikali wakipe kipaumbele zaidi Kiswahili” 

Ameenda mbali zaidi na kuongeza kuwa, “sehemu zote za umma ambazo wananchi wanatumia vema kingetumika Kiswahili kwa sababu mahakamani sheria imeandikwa kwa Kiingereza na mtuhumiwa hafahamu Kiingereza , sasa inakuwa ni ugumu kwake hata ile njia ya kujiteetea anashindwa kwa sababu hajui kimeandikwa nini kwenye ile sheria.”