Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 SEPTEMBA 2023

20 SEPTEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea maoni kuhusu matumizi ya lugha ya kiswahili kutokwa kwa viongozi wanaoshiriki UNGA78, na yaliyojiri hapa makao makuu katika mjadala kuhusu malengo ya maendeleo endelevu. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia hapa makao makuu, kulikoni?  

  1. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki ambaye yuko hapa New York, Marekani kushiriki vikao vya ngazi ya juu vya Umoja wa Mataifa amesema ili kuongeza ushawishi na kukuza lugha ya Kiswahili duniani ambayo sasa inatambulika kimataifa, ni vyema viongozi wa jumuiya hiyo wakawa mfano kwa kuhutubia kwa lugha hiyo mathalani kwenye mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa au UNGA78.
  2. Viongozi wa ulimwengu wanaohudhuria Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wamekuwa na Mjadala wa Ngazi ya Juu kujadili ufadhili kwa ajili ya maendeleo hususan katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewasihi kuitumia fursa ya majadiliano hayo ili kurekebisha mfumo wa ufadhili duniani.   
  3. Na katika makala wakati hapa Makao Makuu hii leo kukifanyika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu tabianchi na jinsi ya kudhibiti athari zake, wakazi wa Kibokoni kaunti ya Kilifi nchini Kenya, wamechukua hatua kwani baada ya kuathirika wamejijengea mnepo na kuendelea kujikimu kimaisha kwa kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki kwenye mabwawa.
  4. Mashinani inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mjadala wa Baraza Kuu kunafanyika mkutano kuhusu hali ya Sudan. Naibu msaidizi wa Katibu Mkuu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Joyce Msuya anasema kwa upande wa kibinadamu hali ni tete. 

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
14'56"