Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

17 NOVEMBA 2022

Hii leo jaridani tunaangazia mada kwa kina na leo tunafunga safari hadi bara Hindi huko nchini India kusikia kuhusu kijiji cha kwanza nchini humo kinachotumia nishati ya sola pekee kwa wakazi wake zaidi ya 6,400.  Pia litakuletea Habari kwa ufupi kama zifuatayo:

Sauti
12'23"
UN

NENO: "MUKU"

Na sasa ni wakati wa kujifunza Kiswahili, ambapo leo mtaalam wetu  Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, anatufafanulia maana ya neno "MUKU"

Sauti
1'4"
UN

Methali: Mwanzo kokochi mwisho nazi

Na leo katika kujifunza Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anatufafanulia maana ya methali, "MWANZO KOKOCHI MWISHO NAZI," karibu!

Sauti
2'4"

27 OKTOBA 2022

Hii leo jaridani ni Mada kwa Kina na tunakuunganisha moja kwa moja na mwenzetu Flora Nducha aliyeko Kigali nchini Rwanda akimulika harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, za kuhakikisha taifa hilo la Afrika Mashariki linatekeleza kwa ufanisi lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu, SDG la afya kwa wote na ustawi ifikapo mwaka 2030.

Hata hivyo kuna Habari kwa Ufupi na Leah Mushi akimulika:

Sauti
11'30"
UN

Neno Kuchakasa

Karibu kujifunza Kiswahili , ambapo leo mtaalam wetu  Onni Sigalla Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , anatufafanulia maana ya neno "KUCHAKASA".

Sauti
41"