Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

Habari za UN

MSEMO - Sikio halilali njaa

Na leo Katika jifunze Kiswahili tuko Baraza la Kiswahili la ZANZIBAR nchini Tanzania ambapo hii leo Dkt. Mwanahija Ally Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA anafafanua msemo “sikio halilali njaa.” 

 

Sauti
1'5"

02 FEBRUARI 2023

Hii leo katika Jarida tunakuletea Habari kwa Ufupi, Mada kwa Kina na Jifunze lugha ya Kiswahili.

Katika Habari kwa Ufupi Leah Mushi anamulika ziara ya Papa Francis nchini DR Congo na wito wake kwa vijana na viongozi wa dini kukataa rushwa. Halikadhalika anamulika maeneo oevu na umuhimu wake bila kusahau nchini Sudan Kusini ambako Umoja wa Mataifa unaendelea kutoa misaada kwa familia zilizokimbia kutoka katika eneo la Pibor.

Sauti
12'

28 NOVEMBA 2022

Hii leo jarida linakuletea habari za WHO na michuano ya fainali za Kombe la Dunia. Makala inatupeleka kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya kusikia simulizi ya msichana mnufaika wa mradi wa Girl Shine na Mashinani tutaelekea nchini Uganda kwa mkimbizi mwanaharakati wa mazingira

Sauti
10'56"

25 NOVENBA 2022

Hii leo jarida linaangazia afya nchini Haiti na ujenzi wa amani hasa kwa lengo la kuepusha vijana kutumbukizwa kwenye vikundi vyenye msimamo mkali huko Garissa nchini Kenya. Makala tunakwenda nchini Poland na Mashinani nchini Ethiopia, kuliko ni?  

Sauti
10'28"

23 NOVEMBA 2022

Hii leo jarida linamulika ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na pia mradi wa kupatia fedha jamii nchini Malawi. Makala tunakwenda nchini Kenya na Mashinani nchini Tanzania.

Sauti
14'25"

22 NOVEMBA 2022

Hii leo jarida linaangazia Mada kwa kina tukimulika kongamano la kimataifa la wataalam wa kifua kikuu au TB lmjini Nairobi, Kenya na habari kwa ufupi ikiangazia kazi za Umoja wa Mataifa nchini Morocco, maandamano nchini Iran na walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.  Na mashinani tutaelekea Visiwa vya Solomoni katika eneo la kusini mwa Bahari ya Pasifiki, huko msemo wa "Majuto Mjukuu" umekuwa dhahiri,  kulikoni?

Sauti
12'5"