Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

18 MACHI 2022

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo Ijumaa Lea Mushi na akuletea pamoja na mambo mengine

-Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP limesema wakati bei za vyakula duniani zimefikia kiwango cha juu kabisa, WFP ina wasiwasi  juu ya athari za vita nchini Ukraine katika uhakika wa upatikanaji chakula duniani.

Sauti
16'52"

15 Machi 2022

Hii leo jaridani Leah Mushi anamulika: Hofu na shaka inayotawala kwa familia zilizoko ukimbizini ndani ya Ukraine huku waume au baba zao wakisalia kwenye mapigano; Wito wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa serikali Myanmar izuie vikosi vyake vya usalama kushambulia raia; Walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wakihudumu Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wapaza sauti wanavyojisikia kuhudumu chini  ya bendera ya UN na mchango wao kwenye amani; Makala anabisha hodi kwenye kongamano la kimataifa la lugha ya kiswahili linaloendelea jijini Arusha nchini Tanzania

Sauti
12'53"

11 Machi 2022

Hii leo jaridani Flora Nducha anakuletea mada kwa kina inayomulika harakati za Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo FAO nchini Tanzania za kuwezesha wanawake kushiriki katika sekta ya uvuvi huko mkoani Kigoma kupitia mradi wa FISH4ACP ambako wanawake wamepaza sauti jinsi  ushiriki wao umesaidia kuinua kipato cha familia.

Sauti
11'14"
UN

Jifunze kiswahili- Neno: Shake

Hii leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Onni Sigalla ambaye ni Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anafafanua maana ya neno, shake.

Anasema shake ni ile hali anayokuwa nayo mtu kama vile furaha au huzuni ya kupitiliza lakini haionekani usoni mwake. Mtu analia kwa kwikwi bila kutoa sauti.

Sauti
1'4"