Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

21 Februari 2022

Leo ni siku ya kimataifa ya lugha mama. Lugha mama ni ile ambayo mtu anaizungumza ya kwanza na inaweza kuwa pale alikozaliwa au ni lugha ya asili ya jamii yake. Kwa wengi wa wakazi wa nchi za Afrika Mashariki, Kiswahili ni lugha mama kwa kuwa inazungumzwa katika nchi zote za eneo hilo na zile za jirani na pia ni lugha ya kufundushia shuleni. Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO linasema maudhui ya mwaka huu ya siku hii ni matumizi ya teknolojia katika kujifunza lugha mbalimbali, fursa na changamoto.

Sauti
12'15"
UN

METHALI: "KUKU HAVUNJI YAILE"

Katika kujifunza Kiswahili tunapata ufafanuzi wa methali "KUKU HAVUNJI YAILE" na mchambuzi wetu ni  Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , BAKITA.

Audio Duration
1'5"
UN

Methali, "Mwendapole Hajikwai"

Karibu kujifunza Kiswahili , leo tunapata ufafanuzi wa maana ya methali, "Mwendapole Hajikwai" na mchambuzi wetu ni Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani.
 

Audio Duration
53"
© UNICEF/Jimmy Adriko

Uganda nayo yachukua hatua kuimarisha matumizi ya lugha ya Kiswahili

Tarehe 23 mwezi uliopita wa Novemba mwaka huu wa 2021, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO liliridhia tarehe 7 mwezi Julai kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya Kiswahili. 
 
Hatua hii imezingatia misingi mbalimbali ikiwemo nafasi ya lugha hiyo katika kuleta utangamano katika jamii, kuwa chanzo cha kipato na hata kusongesha amani na usalama. 
 

Sauti
4'6"
UN News/Anold Kayanda

Siku ya Kiswahili Duniani ni zawadi ya Tanzania kwenda duniani: Balozi Gastorn

Kutangazwa kuwa na siku maalum ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili duniani ni zawadi kubwa kutoka Tanzania kwenda duniani na hii ni furaha kubwa sana amesema mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Profesa Kennedy Gastorn akielezea hisia zake baada ya wiki iliyopita shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kupitisha azimio la kuifanya tarehe 7 Julai kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani. 
(CLIP BALOZI KENENDY) 

30 NOVEMBA 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo miongoni mwa tuliyokuandalia hii leo ni pamoja na vipimo vya VVU vyapungua UNITAID  waomba ufadhili zaidi, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linatumia mabalozi wake watoto ambao ni wachechemuzi kuhusu tabianchi kuelezea adha ambazo watoto wanapata kutokana na madhara ya tabianchi na nini wanataka kifanyike.

Sauti
12'55"