Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lugha ya kiswahili itatusaidia kufanya biashara na kuwasiliana Afrika

Dkt.Peter Mathuki, Katibu Mkuu jumuiya ya Afrika Mashariki
UN News
Dkt.Peter Mathuki, Katibu Mkuu jumuiya ya Afrika Mashariki

Lugha ya kiswahili itatusaidia kufanya biashara na kuwasiliana Afrika

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. Peter Mathuki amesema wakati nchi wanachama wa jumuiya hiyo wakikutana kesho Visiwani Zanzibar nchini Tanzania katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani wananchi wa bara zima la Afrika wajiandae kunufaika na lugha hiyo.

Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Dkt. Mathuki amesema wakati tarehe 7 mwezi Julai dunia ikisheherekea lugha ya Kiswahili tayari lugha hiyo ni lugha rasmi ya mawasilino ya EAC kama ilivyopitishwa katika kikao maalum cha viongozi w anchi wanachama.

“Sisi kama jumuiya tunafuraha sana kwamba tarehe hii tutajiunga na wananchi wa mujuiya ya Afrika Mashariki EAC kokote walipo lakini rasmi kule Zanzibar kusherehekea Kiswahili kama lugha rasmi ya jumuiya.”

Amesema maadhimisho hayo yanategemewa kuhudhuriwa na viongozi wote wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

“Ikiwa ni mara ya kwanza tunaandhimisha siku hii, mwaka huu tutakuwa visiwani Zanzibar lakini kwa miaka inayoendelea tutakuwa tunapanga nchi tofauti ya kusherehekea siku hii

Kiswahili kutumika katika biashara

Dkt Mathuki amesema anafahamu kwamba lugha hii pia imekubalika na Muungano wa Afrika AU kutumika kama lugha rasmi.

“Tunafurahi lugha hii niya ulimwengu mzima na itatusaidia katika kufanya biashara hapa kwetu barani Afrika kwakuwa AU wameitambua si tu kama lugha rasmi bali lugha ya kutumika katika biashara.”

Amesema lugha hii itasaidia pakubwa hasa kwenye ukuaji wa jumuiya na kuelewana kwa mambo tofuati “wananchi wanaweza kuwasiliana baina ya nchi na nchi, wataweza kufanya biashara na kukubaliana kwa kutumia lugha ya Kiswahili.”

Amepongeza na kushukuru shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO kuitambua na kuikubali lugha ya Kiswahili kwa umuhimu wake na kuitengea siku rasmi ya kuadhimishwa tarehe 7 mwezi wa 7.

Amekumbusha watu wote wanaozungumza lugha ya Kiswahili kuendelea kukienzi na kuhamasisha wengine wazungumze lugha hii.