Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiswahili hakijatupa ajira tu bali kinaendesha maisha yetu: Wakaazi Goma DRC

Wakaazi wa DRC wakiwa na katika shughuli zao.
UN News Video/Byobe Malenga
Wakaazi wa DRC wakiwa na katika shughuli zao.

Kiswahili hakijatupa ajira tu bali kinaendesha maisha yetu: Wakaazi Goma DRC

Utamaduni na Elimu

Lugha ya kiswahili inatajwa kuwa chombo chenye nguvu sana kinachoingilia kati ujenzi wa amani na pia katika biashara kwa wakaazi wa mji wa Goma katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Kiswahili ndio lugha ya kwanza nchini DRC  yenye idadi kuwa ya wazungumzaji wa lugha hiyo katika mikoa ya Mashariki na Magharibi mwa nchi na inatumiwa hata kwenye vyombo vya habari kama Redio na televisheni. Lugha hii inaruhusu mawasiliano miongoni mwa wakazi wa sehemu ya Mashariki ya Afrika. 

Mwandishi wa idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, Byobe Malenga amefunga safari hadi maeneo hayo na akashuhudia hali halisi.

Mjini Goma, pilika za kila siku zinaendelea na wakazi wa mji huu wa Goma wakiwemo wafanyabiashara, madereva wa teksi na pia wanahabari wanaelewa umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika jamii ya eneo hili la kivu kasakazini.

Nathanaël Mugenzi ni dereva wa pikipiki.
UN News Video/Byobe Malenga
Nathanaël Mugenzi ni dereva wa pikipiki.

Nathanaël Mugenzi ni dereva wa pikipiki au maarufu kwingineko kama bodaboda kutoka mji wa Goma, anasema kwake lugha ya Kiswahili ni hazina.

Kijana huyu ambaye hajapata nafasi ya kwenda shule anawasiliana vyema kwa Kiswahili na wateja wake kutoka mashariki mwa DRC na wale wanaotoka nchi jirani za Afrika Mashariki anasema Kiswahili kinanisaidia kwa wateja maana tunaelewana kwa mapatano ya bei. wanyarwanda pia wanaongea kwa Kinyarwanda  amchao ndiyo lugha ya mbele ” 

Nathanaël hayuko peke yake katika kuendeleza lugha hii kwani Asaph Muhindo ambaye ni mfanyabiashara wa magodoro anasafiri kati ya Rwanda, Burundi, Tanzania na Uganda, na anasema ameshuhudia umuhimu wa mtaji wa lugha ya Kiswahili katika kazi yake kwa miaka kadhaa.

Asaph Muhindo ni mfanyabiashara wa magodoro.
UN News Video/Byobe Malenga
Asaph Muhindo ni mfanyabiashara wa magodoro.

“Lugha hii inanisaidia sana katika uuzaji wa magodoro hapa kila mteja anaye fika hapa tunazungumza kwa kiswahili na hii ni moja ya vitu vinanifanya kuwashawishi kununua bidhaa zangu. Ninaposafiri kwenda kununua bidha iwe Uganda, Burundi au Tanzania natumia Kiswahili ”

Eneo hilo kuna watu wangine wambao elimu yao ya shule ni chini sana na lugha ya Kiswahili inaamimika kama marejeleo na kiunganishi kati ya watu waliopata nafasi ya kusoma na wengine ambao hawajapata kama anavyosema hapa Mushagalusa Bisimwa, anayeamini kwamba lugha ya Kiswahili ni muhimu barani Afrika na hasa katika eneo lake anasema “Hatuna lugha ingine ambayo tunajuwa isipokuwa kiswhaili. Kwani yule ambaye hakusoma hawezi akaongea kifaransa lakini Kiswahili kimekuwa kikitusaidia sana.” 

Kwa kutambua umuhimu wake Umoja wa Mataifa uliunda “Kitengo cha Lugha ya Kiswahili” ndani ya Redio ya Umoja wa Mataifa, na kufanya Kiswahili kuwa lugha pekee ya Kiafrika iliyopo ndani ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa.

Mustapha Mulonda, ni mwalimu wa sayansi ya habari na mawasiliano katika chuo kikuu, Goma.
UN News Video/Byobe Malenga
Mustapha Mulonda, ni mwalimu wa sayansi ya habari na mawasiliano katika chuo kikuu, Goma.

Mustapha Mulonda, ni mwalimu wa sayansi ya habari na mawasiliano katika chuo kikuu, Goma kwake, anaamini Kiswahili kikiwa lugha inayozungumzwa zaidi barani Afrika, ni njia muhimu ya kuwasilisha utamaduni, elimu na biashara “Kiwwahili kinazungumza na nchi 14 baranai afrika na nje ya Afirka Uarabuni na hata Ulaya wameanaza kujifunza lugha hii. Yaa ni lugha ya kimataifa kwa sasa na inabidi watu kujifunza lugha hii maana wakati tukiwa na mazungumzo katika lugha hii ya Kiswahili ina heshima na maendeleo. UNESCO kukubali Kiswahili ni fahari sana maana inabidi watu wote ulimwenguni waweze kufaidika nayo” 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Kiswahili ni mojawapo ya lugha zinazotumiwa sana katika familia ya Kiafrika, na inayozungumzwa zaidi katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ni kati ya lugha 10 zinazozungumzwa zaidi ulimwenguni, kikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 200. Lugha hii ni mojawapo ya lugha 4 za taifa nchini DRC nay a kwanza kuzungumzwa kwa asilimia 47 kote nchini DRC. Pia inafundishwa katika vyuo vikuu vikuu na vyuo vingine kote ulimwenguni kwa ujumla.