Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kiswahili duniani kuadhimishwa tarehe 7 Julai kila mwaka- UNESCO

Nembo
UN
Nembo

Siku ya Kiswahili duniani kuadhimishwa tarehe 7 Julai kila mwaka- UNESCO

Utamaduni na Elimu

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO leo limeitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Taarifa hiyo imetangazwa leo kwenye makao makuu ya UNESCO mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa twitter wa UNESCO azimio maalum la kuitangaza siku hiyo limepitishwa na wanachama wote bila kupungwa.

Hatua hiyo inakifanya Kiswahili kuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika kutambuliwa na Umoja wa Mataifa na kuwa na siku maalum ya kuadhimishwa.

Kiswahili hadi sasa tayari kinatambulika kama miongoni mwa lugha rasmi kwenye Muungano wa Afrika, na kinatumika kama lugha rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na bunge la Afrika n ani moja ya lugha za Afrika zinazozungumzwa na watu wengi duniani.

Taarifa zaidi kuhusu azimio hili na lina maanisha nini kwa wazungumzaji wa Kiswahili duniani tutakuletea katikia vipindi vyetu vijavyo.