Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Gharama kubwa na huduma duni ni tatizo kwa afya ya jamii

Leo ni siku ya afya duniani, Umoja wa Mataifa waungana na dunia kuadhimisha siku hii ambayo kwa mwaka huu inajikita kupiga darubini masuala ya afya na uzee.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa na afya njema ni chachu ya watu kuishi maisha bora na marefu kwa faina ya familia na jamii zao.

Hata hivyo imekuwa ni mtihani mkubwa kwa watu hasa kutoka nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo umri wa watu kuishi unakadiriwa kutozidi miaka 50.

Msafara wa watu wanaorejea nyumbani umekwama katikati ya mapigano Sudan Kusini:IOM

Shirika la wahamiaji la IOM limesema msafara wa magari yanayosafirisha raia wa Sudan Kusini wanaorejea nyumbani kutoka Sudan Kaskazini umekwama katikati ya mapigano kati ya waasi na majeshi ya Sudan Kusini.

Kwa mujibu wa IOM watu zaidi ya 1000 hadi hivi sasa wanashikiliwa. Shirika la IOM limesema linashirikiana na mashirika mengine kuwaokoa raia hao. Jumbe Omar Jumbe anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Kuadhimisha Siku ya Maji duniani

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya maji ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni "maji na usalama wa chakula" inaonekana kuwa nchi nyingi zimepiga hatua katika udhibiti wa maji lakini bado juhudi zaidi zinahitajika.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova ameitaka dunia kuungana pamoja ili kuhakikisha kila mtu ana fursa ya maji safi na chakula, sasa na baadaye.

Kwa upande wake Wananchi ambao wengi hukabiliwa na matatizo ya maji wanasemaje kuhusu siku hii.

Hawa ni baadhi ya waakazi wa Afrika Mashariki.

Katika kuadhimisha siku ya kupinga matumizi ya tumbaku

Takribani watu milioni 5 wenye umri wa miaka 30 na zaidi wamekufa kutokana na matumizi ya moja kwa moja ya tumbaku kote duniani, na hiyo ni sawa na kifo cha mtu mmoja kila baada ya sekunde sita.

Kwa mujibu wa ripoti  ya WHO maeneo ambayo yana kiwango kikubwa cha vifo vitokanavyo na matumizi ya tumbaku ni Marekani na bara Ulaya ambako tumbaku imekuwa ikitumika kwa muda mrefu zaidi.

Pia ripoti hiyo imebainisha kwamba tumbaku ndio mihadarati pekee iliyohalalishwa ambayo inawaua watu wengi wanaoitumia kama ilivyokusudiwa na wazalishaji.

Mwanamke aliyejitolea kuwasaidia watoto wasichana na wanawake kwa jumla:Mukamabano

Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Wanawake duniani kuna wanawake mbali mbali wanaojitoa kusaidia wanawake wenzao na wasichana. Miongoni mwao ni Marie Claudine Mukamabano kutoka nchini Rwanda ambaye anaishi Marekani. Marie ameanzisha kituo cha kuwalea watoto yatima nchini Rwanda. Yeye ni manusura wa mauaji ya kimbari lakini pia ni mwanzilishi wa kituo cha kulea watoto kiitwacho "Why Do I Exist". Kituo hiki kinawasaidia watoto wasichana na wanawake. Amezungumza na Mkuu wa Idhaaa hii Flora Nducha. Wasikilize...

UM waadhimisha Siku ya Wanawake kwa kupanda mlima Kilimanjaro

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na makundi mengine ya kiharakati pamoja na serikali ya Tanzania umeadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kupanda mlima kulimanjaro kama ishara mojawapo ya kusuma mbele nafasi ya mwanamke huku ikipinga vitendo vya dhulma dhidi yao.

Hii ni mara ya kwanza kwa tukio kama hilo, ambalo pia limewashirikisha vijana kutoka mataifa mbalimbali barani afrika waliopaza sauti zao juu ya kulinda haki za wanawake duniani kote.

Umuhimu na thamani ya mwanamke wa Kijijini

Wiki hii kwenye Umoja wa Mataifa kunafanyika kongamano ambalo linajumuisha wanawake kutoka kila pembe kujadili umuhimu na thamani ya kila mwanamke kijijini. Kongamano hili limeandaliwa na kitengo cha wanawake cha Umoja wa Mataifa UN WOMEN na linashirikisha wanawake viongozi na wanaharakati wa kupigania haki za wanawake na wadau wengine ambao wanachagiza haki za wanawake.

Kongamano la UM juu ya ukuzaji sekta ya madini lafikia tamati Tanzania

Kamishna ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya uchumi kwa kanda ya afrika, imehitimisha mkutano wake wa 16 jijini Dar es salaam ambako imesisitiza haja ya kuimarisha sekta ya madini kwa ajili ya kukuza maendeleo barani humo.

(SAUTI GEORGE NJOGOPA)

Mkutano huo ulioduma kwa muda wa juma moja, umewaleta pamoja mawaziri wa masula ya madini, watunga sera, wawakilishi kutoka nchi za Ulaya, pamoja na makundi mengine ya kimaendeleo.