Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Wakimbizi wa maziwa makuu Tanzania waanza warejea nyumbani

Wakati dunia hii leo inaadhimisha siku ya wakimbizi ambako kunasisitizwa kuepusha madhira yanayoweza kuzalisha watu wa jamii hiyo, idadi kubwa ya wakimbizi kutoka eneo la maziwa makuu sasa wameanza kurejea nyumbani baada ya kuwa uhamishoni kwa kipindi kirefu

Huko nchini Tanzania ambako kwa miaka kadhaa sasa imekuwa ikihifadhi wakimbizi kutoka nchi za Burundi,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Somalia ripoti zinaonyesha kuanza kupungua kwa idadi ya wakimbizi hao walikubali kurejea makwao.

Kutoka Dar es salaam George Njogoa anaripoti zaidi

IOM yaendelea kuahamisha wakimbizi wa Sudan Kusini

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanzisha shughuli ya kuwahamisha wakimbizi kutoka kituo cha Al Damazin kilicho kwenye eneo la magharibi kati ya mpaka wa Ethiopia na Sudan kwenda kambi mpya iliyo eneo la Benishangul Gumuz kaskazini magharibi mwa Ethiopia.

Uamuzi wa kuhamisha wakimbizi hao ulifanywa baada ya kituo hicho ambacho kina uwezo wa kuwahifadhi watu 14,000 kufurika.

Duru ya mwisho mjadala wa Rio+20 imeanza Brazil

Majadiliano ya matokeo ya mwisho ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo endelevu au Rio+20 yako yako katika hata za mwisho.

Majadiliano hayo yanaanza rasmi Juni 20 hadi 22 mjini Rio Dejaneiro Brazili ambako wakuu wan chi na serikali mbalimbali wanatarajiwa kutia saini nyaraka muhimu kwenye mkutano huo.

Mkutano huo pia unahudhuriwa na makundi mbalimbali, wakiwemo wadau wa maendeleo, jumiya ya kidini, wawakilishi wa jumuiya za kijamii na mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s.

Afisa wa UM aahidi msaada kutoka UM kusaidia mkoa wa Kivu

Afisa wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya binadamu katika jamhuri ya kidemokrasia ya congo(DRC), Bw. Fidèle Sarassoro, anaahidi kutoa msaada wa kiutu kwa wahame wa vita vya makundi yenye silaha kwenye mkoa wa kivu mwa kusini. Alisema hayo siku ya Jumanne mei 07/2012 mjini bukavu katika mkutano wake na waandishi wa habari. Mwandishi wetu kutoka Bukavu anaelezea.

(SAUTI YA FIDELE SARASSORO)

Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari

Uhuru wa kujieleza ni moja ya haki muhimu kwa watu, na ni uhuru unaozidi uhuru wa aina yoyote ile na kutoa msingi wa utu wa mtu. Haya yameelezwa katika taarifa ya pamoja ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mkurugenzi wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova. Taarifa yao ikitoa ujumbe maalumu wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari imesema, vyombo vya habari huru, vinavyojumuisha wote na vinavyojitegemea ni muhimu katika kufanikisha azima hii.

Nchi nyingi masikini hazijapa suluhu ya malaria

Wakati ulimwengu umeadhimisha siku ya Malaria bado nchi hasa zilizo maskini hazijapata suluhu kamili na njia mwafaka za kupambana na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.

Bado watu wengi hawana uwezo au hawajapata hamasisho kuhusu njia kamili za kujikinga kutokana na ugonjwa wa Malaria ugonjwa ambao husababisha vifo vingi zaidi kwenye nchi hizi.

Ukosefu wa madawa ya kutibu ugonjwa wa malaria na neti za kujikinga dhidi ya mbu pamoja na madawa ya kutibu neti hizo ni baadhi ya masuala yanayoyatia hatarini maisha ya watu wengi kila siku.