Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umuhimu na thamani ya mwanamke wa Kijijini

Umuhimu na thamani ya mwanamke wa Kijijini

Pakua

Wiki hii kwenye Umoja wa Mataifa kunafanyika kongamano ambalo linajumuisha wanawake kutoka kila pembe kujadili umuhimu na thamani ya kila mwanamke kijijini. Kongamano hili limeandaliwa na kitengo cha wanawake cha Umoja wa Mataifa UN WOMEN na linashirikisha wanawake viongozi na wanaharakati wa kupigania haki za wanawake na wadau wengine ambao wanachagiza haki za wanawake.

Miongoni mwa mada wanazojadili ni jinsi ya kumwezesha mwanamke kijijini kiuchumi, kijinsia na kijamii. Mmoja wa waliohudhuria ni Jane Kiragu kutoka nchini Kenya ambaye amejadili na Monica Morara wa redio ya Umoja wa Mataifa.