Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Maoni kuhusu umuhimu wa Radio ya UM

UM ukiadhimisha siku ya Radio duniani hii leo watu kutoka Afrika wametoa maoni kuhusu umuhimu wa Radio, ikiwemo Radio ya Umoja wa Mataifa. Mwandishi wetu kutoka Tanzania alipata kuzungumza na watu mbali mbali waliotoa maoni tofauti tofauti kuhusu umuhimu wa radio ya Umoja wa Mataifa.

(MAONI KUTOKA TANZANIA)

Mahiga amefurahi sana kwa hatua ya kihistoria ya kuhamisha ofisi yake Somalia

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amesema Alhamisi kuwa amefurahi sana kufanikiwa kuhamisha ofisi yake kutoka mjini Nairobi Kenya na kuiweka mjini Moghadishu Somalia.

Katika waraka maalumu aliowaandikia Wasomali, Mahiga amesema anashukuru msaada mkubwa wa vikosi vya muungano wa Afrika AMISOM na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya siasa kwa ajili ya Somalia UNPOS kufanikisha hilo.

Tanzania inadai maili 350 katika bahari ya Hindi

Tanzania imewasilisha ombi la kuongeza eneo la maili 150 hadi 200 za eneo lililo chini ya udhibiti wake kwenye bahari ya Hindi.

Chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa sheria za bahari wa mwaka 1982, taifa lililo katika mwambao wa bahari lina haki ya kudai eneo ili kuweza kutafuta mali asili kama samaki, madini na mafuta.

Ombi hilo limewasilishwa kwenye Umoja wa Mataifa kwa wahusika wa masuala ya bahari na aliyewasilisha ombi hilo ni waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi wa Tanzania Profesa Anna Tibaujuka.

Misri yataka makubaliano mapya kuhusu matumizi ya mto Nile

Nchi saba zitumiazo maji ya mto Nile, miaka michache iliyopita zilianzisha mkataba mpya unaotaka kuwepo kwa uwiano sawa wa matumizi ya maji ya mto Nile.

Waziri wa mambo ya Nje wa Misri Mohamed Kamel Amr hivi sasa ameanza safari ya kuzitembelea nchi hizo saba kwa ajili ya kuweka ushawishi kabla mkutano wao wiki ijayo Nairobi Kenya.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bwana Bernard Membe, kuna uwezekano sasa pande hizo zikafikia makubaliano yatayozingatia maslahi ya pande zote. George Njogopa anaripoti

(PKG YA GEORGE NJOGOPA)

Siku ya kimataifa ya wahamiaji

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhamiaji Shirika la kimataifa uhamiaji IOM linasema kwamba ukosefu wa huduma za matibabu kwa wahamiaji ni jambo ya kutisha na ina inahitaji kushughulikiwa kwa dharura .  Jumbe Omari Jumbe wa shirika la IOM anafafanua amezungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa.

Siku ya kimataifa ya ulemavu

Ni bayana kwamba watu walemavu huwa wanapitia chamgomoto nyingi za kimaisha zikiwemo umaskini, ajira, ndoa na kusafiri kutoka eneo moja hali lingine.

Siku ya kimataifa ya walemavu inapoadhimishwa hapo kesho December 3, Jason Nyakundi wa Radio ya Umoja wa Mataifa amepata kuzungumza na Isaac Manyonge mhasibu ambaye amekuwa mlemavu tangu utotoni na kisha kutuandalia makala ifuatayo. Tega sikio….

(MAZUNGUMZO YA JASON NYAKUNDI NA ISAAC MANYONGE)

Kila mmoja anajukumu la kumlinda mwenzie na ukimwi

Katika siku ya ukimwi duniani wito umetolewa kwa kila mtu kubeba jukumu la kujilinda na kuwalinda wengine na maambukizi mapya ya ukimwi.

kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO na lile la kupambana na ukimwi UNAIDS kila mtu katika jamii zote duniani ana fursa ya kuchangia kuhakikisha kuna maambukizi mapya sufuri, unyanyapaa sufuri na vifo vitokanavyo na ukimwi sufuri.

Wanaanchi hawa wa Afrika wana maoni gani kuhusu siku hii? wasikilize

(MAONI KUHUSU SIKU YA UKIMWI)

Wananchi wa DR Congo milioni 32 wapiga kura leo

Wananchi milioni 32 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  wameshiriki hii leo katika uchaguzi mkuu ulioshuhudia wagombea 11 wakiwania wadhifa wa urais akiwemo rais anayeondoka madarakani Joseph Kabila na mpinzani wake mkuu Etienne Tchisekedi.

Vilevile wagombea elfu 18 wamejitokeza kuwania nafasi 500 pekee za ubunge. Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga amefuatilia siku ya kwanza ya upigaji kura na kutuandalia taarifa hii.

(RIPOTI YA RAMADHAN KIBUGA)

Mamia ya wakimbizi wa Ivory Coast na Angola warejea nyumbani:IOM

Mamia ya wakimbizi ambao walihama makwao kutokana na mzozo wa uchaguzi ulioikumba Ivory Coast wameanza kurejea nyumbani kwa usaidizi wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Pia shirika hilo  linaendelea kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa Angola walioko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia kurundi nyumbani kwa hiyari yao.

Afisa wa IOM Jumbe Omari Jumbe anafafanua kuhusu jitihada hizo alipozungumza na Monica Morara wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.

(MAHOJIANO NA JUMBE OMARI JUMBE)

Ugonjwa wa kisukari unaweza kuzuilika:UM

Shirikisho la kimataifa la maradhi ya Kisukari IDF na shirika la afya duniani WHO wanasema maradhi ya kisukari yanaweza kuzuuilika kwa watu kuzingatia masharti ikiwemo kula vyakula vinavyofaa, kufanya mazoezi, kupungza unene na kuepuka matumizi ya tmbaku.

Leo ikiadhimishwa siku ya kisukari duniani takwimu zinaonyesha kuwa watu takribani milioni 4 wanakfa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa kisukari na wengi wao wanatoka nchi za kipato cha wastani na kipato cha chini.