Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

02 NOVEMBA 2022

Hii leo katika Habari za UN Assumpta Massoi anamulika masuala yafuatayo:

1. Ukame uliolighubika eneo la Pembe ya Afrika kwa miongo minne mfululizo umesababisha changamoto kubwa kwa mamilioni ya raia wa hilo ikiwemo Kenya, Ethiopia na zaidi Somalia ambako  maeneo mengi yanakabiliwa na kutokuwa na uhakika wa chakula na hatihati ya kutumbukia kwenye baa la njaa. Mashirika ya misaada ya kibinadamu likiwepo la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP yako msitari wa mbele kuwasaidia watu wenye uhitaji hususani wa chakula.

Sauti
12'23"

01 NOVEMBA 2022

Hii leo katika Habari za UN kubwa ni Mada kwa Kina ikimulika ni kwa namna gani wavumbuzi wanasakwa duniani ili kufanikisha lengo namba 9 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs la kutaka uvumbuzi, ugunduzi kwa ajili ya maendeleo endelevu. Leah Mushi amezungumza na Andrew Minja, Afisa kutoka kampuni ya Ye2 ambayo kazi yake ni kusaka uvumbuzi na ugunduzi bila kusahau kuhakikisha wavumbuzi hao wananufaika na kazi zao za kufanya dunia kuwa pahala bora zaidi kwa kila mtu.

Habari kwa ufupi zinasomwa kwako na Flora Nducha akimulika:

Sauti
14'3"

27 OKTOBA 2022

Hii leo jaridani ni Mada kwa Kina na tunakuunganisha moja kwa moja na mwenzetu Flora Nducha aliyeko Kigali nchini Rwanda akimulika harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, za kuhakikisha taifa hilo la Afrika Mashariki linatekeleza kwa ufanisi lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu, SDG la afya kwa wote na ustawi ifikapo mwaka 2030.

Hata hivyo kuna Habari kwa Ufupi na Leah Mushi akimulika:

Sauti
11'30"

25 OKTOBA 2022

Hii leo kwenye Jarida la Umoja wa Mataifa tunakuletea mada kwa kina ikimulika filamu ya chapa tatu iliyotengenezwa na taasisi ya Tai Tanzania kuhusu haki za binadamu yeyote yule wakiwemo watu wenye ualbino, Mtoto Njaro ana uwezo mkubwa wa ubunifu, anakutana na changamoto kwenye jamii yake lakini hakati tamaa, anasonga mbele hadi anaibuka mshindi.

Kuna habari kwa ufupi kutoka kwake Flora Nducha akimulika:

Sauti
12'48"

24 OKTOBA 2022

Hii leo Jarida la UN linamulika siku ya Umoja wa Mataifa ambao leo unatimiza miaka 77 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945 huko Francisco nchini Marekani na kukuchambulia zaidi:

Sauti
13'

21 OKTOBA 2022

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia Rwanda ambako Flora Nducha anafuatilia maadhimisho ya miaka 60 ya taifa hilo kwenye Umoja wa Mataifa, kisha anakwenda Tanzania ambako Stella Vuzo amemulika ziara ya Malkia Maxima wa Uholanzi ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ujumuishaji kifedha. Makala tunakwenda Zambia kumulika ni kwa vipi watoa huduma za kijamii wa kujitolea wanaepusha ndoa na mimba za utotoni.

Sauti
12'45"

20 OKTOBA 2022

Hii leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa tuna Mada kwa Kina ikimulika harakati za kutokomeza ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika kupitia elimu ya watu wazima au ngumbaru huko nchini  Kenya. Tayari wanufaika wameanza kuona matunda. Thelma Mwadzaya anakupitisha katika mtaa wa mabanda wa Kiambiu, huko Eastleigh jijini Nairobi.

Sauti
11'33"