Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 OKTOBA 2022

20 OKTOBA 2022

Pakua

Hii leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa tuna Mada kwa Kina ikimulika harakati za kutokomeza ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika kupitia elimu ya watu wazima au ngumbaru huko nchini  Kenya. Tayari wanufaika wameanza kuona matunda. Thelma Mwadzaya anakupitisha katika mtaa wa mabanda wa Kiambiu, huko Eastleigh jijini Nairobi.

Habari kwa ufupi inamulika usaidizi wa WFP kwa Somalia, ziara ya Priyanka Chopra-Jonas, balozi mwema wa UNICEF huko Turkana nchini Kenya, halikadhalika ziara ya Katibu Mkuu wa UN nchini India, Antonio Guterres alikozindua mtindo bora wa maisha wa kuwezesha kuhifadhi sayari dunia.

Na leo kujifunza kiswahili tunakuletea methali isemayo,  Paka hakubali kulala chali, mchambuzi ni Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa BAKIZA, Zanzibar nchini Tanzania.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
11'33"