Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 OKTOBA 2022

25 OKTOBA 2022

Pakua

Hii leo kwenye Jarida la Umoja wa Mataifa tunakuletea mada kwa kina ikimulika filamu ya chapa tatu iliyotengenezwa na taasisi ya Tai Tanzania kuhusu haki za binadamu yeyote yule wakiwemo watu wenye ualbino, Mtoto Njaro ana uwezo mkubwa wa ubunifu, anakutana na changamoto kwenye jamii yake lakini hakati tamaa, anasonga mbele hadi anaibuka mshindi.

Kuna habari kwa ufupi kutoka kwake Flora Nducha akimulika:

  • Kuelekea mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP27 huko Sharm el Sheikh nchini Misri barani Afrika yaelezwa kuwa  athari za mabadiliko ya tabianchi kwa watoto katika kipindi cha kuanzia sasa mpaka mwaka 2050 yatakuwa makubwa. 
  • Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kanda ya Afrika limesema mazingira wezeshi, uwekezaji na utashi wa kisiasa vinaweza kubadilisha mwelekeo wa changamoto za afya ya uzazi na masuala ya ngono (SRHR) nchini Zimbabwe na Afrika kwa ujumla.  
  • Na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limesema linatiwa hofu kubwa na kitendo cha serikali ya Malaysia kuendelea kuwarudisha nchini mwao waomba hifadhi kutoka Myanmar hali inayoweka maisha yao hatarini.  

Na mashinani tunabisha hodi nchini Msumbiji kwa mhamasishaji wa utoaji wa chanjo dhidi ya Polio. Karibu na  mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

 

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
12'48"