Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 OKTOBA 2022

27 OKTOBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani ni Mada kwa Kina na tunakuunganisha moja kwa moja na mwenzetu Flora Nducha aliyeko Kigali nchini Rwanda akimulika harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, za kuhakikisha taifa hilo la Afrika Mashariki linatekeleza kwa ufanisi lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu, SDG la afya kwa wote na ustawi ifikapo mwaka 2030.

Hata hivyo kuna Habari kwa Ufupi na Leah Mushi akimulika:

  • Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO linakadiria kuwa watu milioni 10.6 waliugua kifua kikuu (TB) mwaka 2021, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.5 kutoka mwaka 2020, na watu milioni 1.6 walikufa kutokana na TB kati yao watu 187,000 wakiwa na  Virusi Vya UKIMWI.
  • Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP imebaini kuwa jamii ya kimataifa bado inashindwa kufikia viwango vya kudhibiti ongezeko la joto lisizidi nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha selsiyasi kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi. 
  • Na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kutokomeza Ubaguzi dhidi ya Wanawake inatoa wito kwa mataifa kuunda mara moja, na kutekeleza sera za kina zitakazo linda haki za binadamu za wanawake na wasichana wa jamii za asili kila mahali.

Na leo katika kujifunza lugha ya kiswahili tunakwenda Zanzibar Tanzania kwake Dkt.Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA akichambua methali, Mchama ago hanyele, huenda akawia papo!

 

Karibu na mwenyeji wako leo ni Assumpta Massoi.

 

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
11'30"