Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 OKTOBA 2022

21 OKTOBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia Rwanda ambako Flora Nducha anafuatilia maadhimisho ya miaka 60 ya taifa hilo kwenye Umoja wa Mataifa, kisha anakwenda Tanzania ambako Stella Vuzo amemulika ziara ya Malkia Maxima wa Uholanzi ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ujumuishaji kifedha. Makala tunakwenda Zambia kumulika ni kwa vipi watoa huduma za kijamii wa kujitolea wanaepusha ndoa na mimba za utotoni. Mashinani ni moja kwa moja hadi India ambako huko Katibu Mkuu wa  UN ameshuhudia kijiji kimoja cha watu 6,400 wote wakitumia nishati ya jua kama chanzo cha nishati.Karibu!

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
12'45"