Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

02 NOVEMBA 2022

02 NOVEMBA 2022

Pakua

Hii leo katika Habari za UN Assumpta Massoi anamulika masuala yafuatayo:

1. Ukame uliolighubika eneo la Pembe ya Afrika kwa miongo minne mfululizo umesababisha changamoto kubwa kwa mamilioni ya raia wa hilo ikiwemo Kenya, Ethiopia na zaidi Somalia ambako  maeneo mengi yanakabiliwa na kutokuwa na uhakika wa chakula na hatihati ya kutumbukia kwenye baa la njaa. Mashirika ya misaada ya kibinadamu likiwepo la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP yako msitari wa mbele kuwasaidia watu wenye uhitaji hususani wa chakula.

2. Takriban watoto milioni 3 wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini Sudan, wanakabiliwa na utapiamlo, ambapo kati yao 650,000 wanakabiliwa na utapiamlo mkali sana.  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linafanya kila juhudi ili kuwasaidia watoto hawa kama anavyosimulia.

3.Makala: Ttunakwenda Arusha nchini Tanzania kusikia wanufaika wa mafunzo yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuimarisha matumizi ya eneo huru la biashara barani Afrika.

4. Mashinani: T

tunabisha hodi jimbo la Kusini mwa Rwanda katika wilaya ya Huye kwake Vital Migabo mbaye ni mkuu wa tarafa ya Tumba  akieleza kwa nini ameona umuhimu wa kujifunza lugha ya Kiswahili. 

Karibu!

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
12'23"