Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

15 DESEMBA 2022

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tukimulika ukuaji wa lugha ya Kiswahili nchini Rwanda. Na habari kwa ufupi kutoka nchini Thailand, Ukraine na DR Congo. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt. Josephat Gitonga atafafanua maana ya methali “Usishindane na kari, kari ni mja wa Mungu”.

Sauti
12'36"

14 DESEMBA 2022

Jaridani leo tunakuletea habari kutoka Kenya na DR Congo, makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinanio tunakuletea ujumbe kuhusu wanawake kushirikishwa katika shughuli za ulinzi wa amani.

Sauti
12'15"

13 DESEMBA 2022

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina tukimulika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa kimataifa wa bayoanuai CBD unaoendelea mjini Montreal Canada. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kutoka huko huko Montreal Canada, nchini Somalia na nchini Haiti. Mashinani tunakuletea ujumbe wa mwanauchumi mashuhuri duniani Sir Partha Dasgupta, anasemaje?

Sauti
11'18"

08 DESEMBA 2022

Hii leo jaridani tunaangazia mada kwa kina tukimulika harakati za utalii endelevu Tanzania sambamba na umuhimu wa mnepo katika kujikwamua kiuchumi majanga yanapotekea. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti kuhusu malaria, mkutano wa COP 15 na usafirishaji haramu wa binadamu. Pia tutajifunnza lugha ya Kiswahili tukichambua methali “Mkosa titi la mama, hata la mbwa hulamwa”, karibu!

Sauti
13'19"

07 DESEMBA 2022

Hii leo jaridani tuanamulika Upper Nile nchini Sudan Kusini na nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani tunakuletea ujumbe. Kuhusu ukatili wa kijinsia.

Sauti
12'53"

06 DESEMBA 2022

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tukiwa tungali katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana duniani, tunamulika wale wanaowapokea manusura wa ukatili wa kijinsia nchini Kenya. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani kutoka Uganda.

Sauti
12'13"

02 DESEMBA 2022

Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya WHO, habari kutoka Rwanda, makala inayomulika harakati za Umoja wa Mataifa za kusaidia wakulima wenye ulemavu na mashinani tunakwenda nchini Burkina Faso.

Sauti
11'42"